Wednesday , 1 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu aonya wazazi chanzo mmomonyoko wa maadili kwa watoto
Habari Mchanganyiko

Askofu aonya wazazi chanzo mmomonyoko wa maadili kwa watoto

Spread the love

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Mlima wa Bwana, Slivanus Komba amesema wazazi na walezi wanachangia kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili kwa watoto. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 13 Machi, 2022 katika ibada maalumu ya Jumapili iliyokuwa na lengo la kutubu kwa ajili ya kuomba rehema za Mungu, kwa viongozi wa dini, wahumini na Taifa kwa ujumla.

Amesema wazazi wengi wamewafanya watoto wao kama sehemu ya ziada kwani hawana muda wa kutosha kuzungumza nao wala kujua mienendo yao.

Amesema kibaya zaidi hata watoto wamekuwa hawahimizwi katika kujifunza maneno ya Mungu jambo ambalo linawafanya kuwa watoto wasiokuwa na hofu ya Kimungu.

Askofu Komba amesema umefika wakati wa watu kuomba toba na kuzaliwa upya kwa lengo la kumtumikia Mungu ikiwa ni pamoja na kuliweka taifa pamoja pasipo kuwepo kwa migawanyiko ya kiimani wala kisiasa.

Pia amesema viongozi wa dini pamoja na Serikali kuna namna ambavyo wamekuwa wakifanya kazi kwa kutumia akili zao wenyewe bila ya kumshirikisha Mungu na kusababisha kuwepo na magumu mbalimbali hivyo umefika wakati wa kutubu na kuanza maisha upya.

Aidha, amesema sababu kubwa ya kuyumba ni kutokuwa na bidii ya kusimama katika maandiko matakatifu ya Kimungu na matokeo yake wamekuwa wakichukulia masuala ya Mungu kama mambo ya hiari.

Akizungumzia kumomonyika kwa maadili kwa watoto na vijana, Askofu Komba amesema wazazi na walezi wanachangia kwa kiasi kikubwa kutokana na kutowahimiza watoto kwenda katika sehemu za ibada kujifunza neno la Mungu.

“Tumekuwa tukishuhudia wazazi wengi pamoja na walezi wakiwaacha watoto wao majumbani na wakati mwingine kuwafanya kama walinzi wa nyumba badala ya kuwahimiza kwenda ibadani.

“Ukweli ni kwamba msipowapeleka watoto makanisani ili kujifunza neno la Mungu au kuwahimiza kwenda kanisani mwisho wake watajikuta wanaingia kwenye makundi hatarishi na mwishowe kuharibikiwa” ameeleza Askofu Komba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!