Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba hatari, Ibenge hafui dafu kwa Mkapa
MichezoTangulizi

Simba hatari, Ibenge hafui dafu kwa Mkapa

Spread the love

 

BAO la dakika 42, lililowekwa kamabi na Pape Ousamne Sakho dhidi ya RS Berkane, lilitosha kuifanya klabu ya Simba kuwa kileleni kwenye msimamo wa kundi D, mara baada ya kufikisha alama 7. Anaripoti Kelvin , Dar es Salaam … (endelea).

Sakho ambaye amepachika bao lake la pili kwenye hatua ya makundo ya kombe la Shirikisho, lilitosha kuwafanya Simba kuondoka na pointi tatu muhimu mara baada ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini nchini Morocco.

Mchezo huo wa kundi D, umepigwa hii leo, tarehe 13 Machi 2022, majira ya saa 10 jioni kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar ea Salaam.

Huu unakuwa mchezo wa pili wa Simba nyumbani, mara baada ya kucheza michezo miwili ugenini dhidi ya RS Berkane ambao walipoteza kwa maba 2-0, na mchezo dhidi ya USGN ambao walitoka sare ya bao 1-1.

RS Berkane wamepoteza mchezo huo, wakiwa chini ya kocha wao mkuu Frelent Ibenge ambaye hajawahi kupata matokeo ya ushindi dhidi ya Simba kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Akiwa na kikosi cha AS Vita cha nchini Jamhuri ya Congo, Ibenge kwa nyakati tofauti hakuwahi kupata matokeo ya ushindi mbele ya Simba wakiwa nyumbani.

 

Mara ya kwanza kocha huyo kupoteza mchezo mbele ya Simba akiwa na kikosi cha AS Vita, ilikuwa tarehe 16 Machi 2019 kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa kupokea kichapo cha mabao 2-1.

Kichapo cha Pili kwa Ibenge mbele ya Simba kwenye dimba la Benjamin Mkapa, ilikuwa tarehe 3 Aprili 2021, kwenye hatua ya makundi kwa kukubali kichapo cha mabao 4-1.

Hiki kinakuwa kichapo cha tatu kwa kocha huyo, mbele ya Simba akiwa na timu mbili tofauti kwenye michuano ya kimataifa.

Mara baada ya ushindi wa leo, Simba itasafiri hadi nchini Benin ambapo italwenda kuvaana na ASEC Mimosas kwenye mchezo ujao wa kundi D.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

error: Content is protected !!