KATIKA kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapindizi Zanzibar za kumaliza tatizo la udumavu kwa watoto kampuni ya Asas Dairies imezindua programu ya unywaji wa maziwa kwa wanafunzi wa shule visiwani hapa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar …(endelea).
Uzinduzi wa Programu hiyo unefanyika jana tarehe 26 Agosti 2023 na Ahmed Salim Asas Mkurugenzi wa kampuni hiyo mbele ya Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi aliyeonesha kufuhishwa na mpango huo wenye lengo kuimarisha afya za wananchi wote.
Ahmed Asas alimueleza Rais Mwinyi kuwa kwa kuanzia wamepanga kugawa zaidi ya lita 5,000 kwenye Shule zaidi ya 25 visiwani hapa.
Alisema hatua hiyo imekuja kufuatia ripoti ya mwaka jana iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuonyesha asilimia 1.8 ya watoto Zanzibar wana tatizo la udumavu jambo lililowapalekea kushirikiana na Wizara ya Afya na Wizara ya Elimu kufanya jitihada za kupunguza na ikiwezekana kumaliza tatizo hilo.
Pamoja na hayo alisema lengo lingine la program hiyo ni kuimarisha lishe na Afya za Wanafunzi na Wananchi kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa mwaka mtu Mmoja anatakiwa kunywa Maziwa yasiyopungua lita 200 lakini kwa sasa takwimu zinaonyesha hali ya unywaji maziwa nchini sio ya kuridhisha.
Leave a comment