Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari ARU yabuni teknolojia ya ujenzi rafiki kwa mazingira
Habari

ARU yabuni teknolojia ya ujenzi rafiki kwa mazingira

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Dk. Given Mhina akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mary Maganga (katikati), na Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Adolf Ndunguru (Kulia) wakati wa maonyesho ya bidhaa wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Dodoma jana
Spread the love

CHUO Kikuu Ardhi (ARU), kupitia Taasisi yake ya Utafiti ya Nyumba wamebuni teknolojia ya ujenzi wa gharama nafuu kwa kutumia matofali  ambayo ni rafiki kwa mazingira. Anaripoti Na Mwandishi Wetu…(endelea)

Hayo yalibainika jana wakati wa maonyesho ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yanayoendelea kwenye viwanja vya kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.

Akizungumza kuhusu teknologia hiyo jana, Mhadhiri wa ARU Dkt. Given Mhina alisema matumzi ya tofali za aina hiyo zitasaidia kupunguza hewa ya ukaa duniani, kutunza na kuhifadhi mazingira.

Alisema tofali hizo hutengenezwa kwa kutumia udongo wa mfinyanzi, saruji na maji kidogo .Tofali hizo ni imara kwa matumizi mbalimbali ya shughuli za ujenzi.

Mhandisi wa Ujenzi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Twimanye John, akionyesha teknolojia rahisi ya kutengeneza tofali ambazo ni rafiki kwa mazingira kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yanayofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center mkoani Dodoma

“Tumekuja na teknojia hii kama sehemu ya jitihada ya kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa unaotokana na shughuli za ujenzi na mali ghafi zake kama vile saruji, mchanga na maji…. tunatumia udongo wa mfinyanzi na wakati mwingine vumbi linalotokana na utengenezaji wa kokoto,” alisema

Alisema ujenzi wa nyumba kwa kutumia tofali hizo hauhitaji saruji, mchanga wala maji kwani zinafungamana zenyewe isipokuwa wakati wa kuweka nguzo za nyumba pekee.

Dkt. Mhina alisema hata wakati wa umaliziaji wa nyumba mtu aliyetumia tofali hizo halazimiki plasta ya saruji na mchanga badala yake mafundi watatumia mchanga na saruji kidogo sana kuziba mashimo na kisha mwonekano wa nyumba kuwa wa kuvutia.

Mhandisi wa Ujenzi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Twimanye John, akielezea teknolojia rahisi ya kutengeneza tofali ambazo ni rafiki kwa mazingira kwa wageni waliofika kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yanayofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center mkoani Dodoma

Mtaalamu huyo alisema faida nyingine ya matumizi ya matofali ya aina hiyo ni kutosababisha joto ndani ya nyumba kulinganisha na matofali mengine yaliyozoeleka kwenye shughuli za ujenzi.

“Tofali zinazotengenezwa kwa kutumia saruji na mchanga zinatabia ya kufyonza joto wakati wa mchana na joto hilo kutoka wakati wa usiku lakini mfinyanzi unaotumika kutengeneza tofali hizi unasababisha ubaridi kwasababu hauna tabia ya kufyonza joto,” alisema

“Ndiyo sababu kwenye chungu kilichotengenezwa kwa mfinyanzi ukiweka maji hata mchana wakati wa joto kali baada ya muda maji yanapata ubaridi na watu wengi wamekuwa wakitumia vyungu vya mfinyanzi kupata maji baridi,” alisema

Mhandisi wa Ujenzi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Twimanye John, akielezea teknolojia mbalimbali zilizobuniwa na Taasisi ya Utafiti wa Nyumba ya ARU kwa wageni waliofika kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yanayofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center mkoani Dodoma

Dkt. Mhina alimalizia kwa kusema kuwa Taasisi ya Utafiti wa Nyumba ya ARU imekuwa ikifanya tafiti kwa vifaa vya ujenzi vinavyopatikana hapa nchini na kwingineko duniani.

Aliseama jukumu lingine la taasisi hiyo ni kuhakikisha matokeo ya tafiti wanazofanya zinawafikia walengwa kukuza na kuendeleza matumizi ya vifaa bora vya unjenzi nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!