Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Try Again: Simba tunarudi kwa kishindo
Michezo

Try Again: Simba tunarudi kwa kishindo

Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu ya Simba nchini Tanzania, Salim Abdallah maarufu ‘Try Again’ amesema, wamejipanga kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi hicho katika msimu ujao wa mashindano 2022/23. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Try Again amesema hayo leo Ijumaa tarehe 3 Juni 2022 katika mahojiano maalum na Azam TV akizungumzia masuala mbalimbali yaliyojitokeza ndani ya timu hiyo iliyopoteza ubingwa wa Kombe la Shirikisho.

Aidha, ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyokuwa inaushirikia kwa miaka minne mfululizo unakwenda kwa watani zao Yanga ambao wamebakiza pointi tatu kutangaza ubingwa.

Mwenyekiti huyo amesema, amekwisha kuzungumza na mwenyekiti wa timu hiyo, Bilionea Mohamed Dewji ‘MO’ ambaye amemhakikishia wanakwenda kufanya usajili bora na wa kishindo utakaowawezesha kufanya vizuri kwenye michuano ijayo ikiwemo ya kimataifa.

“Tunarudi kwa kishindo. Tunarudi kwa kishindo na nimezungumza na mwekezaji wetu kuwa atasajili, tutawekezaji kwenye miundombinu, kikubwa tunaomba wapenzi wa Simba tumpe ushirikiano lakini tunawaahidi tunarudi kwa kishindo,” amesema Try Again.

“Sasa ni wakati wa kufanya mabadiliko ya kikosi, tunasajili vizuri, tutabaki na wachezaji wazuri, kuna wengine umri umekwenda na viwango vimeshuka lakini hatutawaacha vibaya, tutazungumza nao na wengine mikataba imemalizika. Tunawashukuru sana wachezaji na benchi la ufundi hadi hapa walipotufikisha,” amesema.

Amesema duniani kote hakuna timu ambayo inachukua makombe miaka yote hivyo msimu huu wao wanapitia nyakati ambazo ni za kawaida kwenye soka.

Kuhusu mrithi wa Kocha Pablo Martin aliyefungashiwa vilago hivi karibuni amesema, “tumekwisha kupokea CV mbalimbali na tunaendelea na uchambuzi ili kumpata mtu sahihi na hivi karibuni tutamtangaza kocha huyo.”

Ametumia fursa hiyo kuwaonya wajumbe wenzake wa bodi ya wakurugenzi ambao wametoka na kwenda kuzungumzia masuala mbalimbali kwenye vyombo vya habari na kuwaomba watumie njia sahihi kushauri.

“Nawashauri viongozi wenzangu, ni vizuri kushauri lakini tutumie njia bora. Kwa nini tulipofanya vizuri nyuma hawakusema. Haipendezi wajumbe wa bodi wana nafasi ya kushauri lakini wanatoka wanakwenda kuzungumza huko nje, si jambo jema,” amesema

Vilevile, amemshauri Mbunge wa Nzega Vijijini (CCM), Dk. Hamis Kigwangalla kutumia njia sahihi kuwasilisha ushauri wake ikiwemo kuonaa na Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi ambaye ni mjumbe wa bodi ya Simba.

“Tumemsikia Kingwalla na hatuzuii mtu kuzungumza, tumepokea ushauri wake na tutautumia lakini ni vizuri kusema mapema, kwa nini anasubiri kusema…. pale bungeni kuna Rashid Shangazi ni mjumbe wa bodi angeweza kuwasilisha ushauri wake,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!