Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki ya NBC yatoa gawio la Shilingi bilioni 4.5 kwa serikali
Habari Mchanganyiko

Benki ya NBC yatoa gawio la Shilingi bilioni 4.5 kwa serikali

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza kwenye hafla hiyo.
Spread the love

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba amepokea gawio la shilingi bilioni 4.5 linalotokana na uwekezaji wa Serikali ndani ya Benki ya NBC. Serikali inamiliki asilimia 30 ya hisa za Benki hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza katika hafla hiyo Dk. Nchemba aliipongeza Benki ya NBC kwa kutoa gawio kwa Serikali na kuakisi mafanikio ya sera ya ubinafsishaji ya serikali iliyolenga kubinafsisha mashirika ya umma ili kuyaongezea tija na ufanisi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi akizungumza kwenye hafla hiyo.

“Serikali inajivunia mafanikio ya Benkl ya NBC kwani Benki hii ni moja ya mashirika ya kwanza kabisa kubinafisihwa nchini. Gawio hili la shilingi bilioni 4.5 mnalolitoa leo ni zaidi ya mara tatu ya gawio mlilotoa mara mwisho, hiki ni kiashiria tosha kwa Serikali kuwa Benki yetu ya NBCipo katika mstari sahihi”, alisema Dkt. Nchemba.

Waziri Nchemba pia alipongeza Benki ya NBC kwa matokeo mazuri ya fedha ambapo ilipata faida ya shilingi bilionin 60 ambalo ni ongezeko la asilimia 702 kwa matokeo ya mwaka 2020. Vilevile, Waziri Nchemba alipongeza jitihada za Benki ya NBC katika kuchangia maendeleo ya Taifa ikiwamo ulipaji wa kodi ambapo mwaka jana ililipa jumla ya shilingi bilioni 20 kama kodi.

Waziri wa Fedha na Mipango Dokta Mwigulu Nchemba (wa tatu kushoto) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni 4.5 kutoka Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa pili kulia) ikiwa ni gawio kutoka linalotokana na uwekezaji wa Serikali ndani ya benki hiyo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dodoma hii leo. Wengine ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu- Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru (Wa pili kulia) na viongozi wengine waandamizi.

“Napongeza sana mchango wenu katika uchumi wa taifa. Hakika nyinyi ni mfano wa kuigwa. Uwekezaji wenu katika jamii umekuwa chachu kubwa ya maendeleo. Napongeza sana sera yenu katika msaada kwa jamii ikiwemo uwekezaji katika ligi ya soka ya mpira ya NBC Premier leaguena uandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon ambazo zinalenga kukusanya fedha za kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya kizazi kwa wanawake” alisema Dkt.Nchemba.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi aliishukuru serikali, kwa kuendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini ambazo zimepelekea Benki kufanya vyema sokoni.

”Faida hii ambayo Benki ya NBC imepata na kuwezesha ulipaji huu wa gawaio la serikali, ina akisi mazingira bora ya biashara nchini. Tunajivunia pia kuweza kulipa kodi ya zaidi ya shilingi bilioni 20 kwa mwaka 2021 na kusaidia kupatikana ajira nyingi kupitia uwekezaji wetu katika ligi ya mpira nchini ya NBC Premier league.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba (katikati) Naibu Katibu Mkuu- Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru (Wa tatu kushoto) na viongozi wengine waandamizi wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw Theobald Sabi (wa pili kulia)

Akizungumzia kuhusu mchango wa Benki kwenye ustawi wa jamii, Sabi alisema” kupitia sera yetu ya msaada kwa jami, tunajivunia kuwekeza katika kutatua changamoto nyingi za jamii ikiwemo uandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon zenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya saratani ya shingo za kizazi kwa wanawake” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!