RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake itafanyia kazi mambo yaliyoibuliwa katika Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 28 Machi 2024, Ikulu jijini Dodoma baada ya kupokea ripoti hizo alizokabidhiwa na CAG Charles Kichere na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni.
“Ripoti hizi zinazosomwa kila mwaka zinachangia maboresho au kuimarisha utendaji ndani ya serikali na mashirika ya umma, kuna dosari zilizotolewa hapa tutaenda kuzifanyia kazi kisawasawa turekebishe na mwakani pengine hizi hazitajirudia tutakuwa tumesogea,” amesema Rais Samia.
Aidha, Rais Samia amesema ripoti hizo zinaonesha kwamba kuna maboresho yaliyofanyika katika masuala ya usimamizi wa fedha za umma kwani ripoti ya CAG imeonesha hati safi zimeongezeka hadi kufikia asilimia 99, wakati hati chafu ikiwa ni moja.
Ripoti ya CAG imeibua madudu katika baadhi ya mashirika ya umma na mamlaka za serikali za mitaa.
Leave a comment