Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Biashara Airtel Tanzania yailipa Serikali Bil. 143
Biashara

Airtel Tanzania yailipa Serikali Bil. 143

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Airtel Tanzania, Gabriel Malata
Spread the love

KAMPUNI ya Airtel Tanzania inayomilikiwa kwa ubia kati ya Serikali na sekta binafsi imetoa gawio la Sh 143 bilioni kwa Serikali kama faida ya kumiliki hisa 49. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya hundi ya malipo ya gawio hilo leo Jumanne tarehe 12 Aprili, 2022, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Airtel Tanzania,  Gabriel Malata, amesema gawio hilo ni la mwaka 2021.

Akifafanua zaidi Malata amesema kiasi hicho kinahusisha Sh 88 za gawio la faida, Sh 43 bilioni malipo ya mauzo ya minara, na Sh 12 bilioni kwaajili ya kuisaidia Serikali katika kazi zake.

Amesema ndani ya miaka mitatu Airtel imeilipa Serikali Sh 36 bilioni ambacho ni jumla ya Sh bilioni moja ambayo Airtel inapaswa kuilipa Serikali kila mwaka kusaidia utekelezaji wa shughuli zake.

Pia amesema imelipa gawio la Bil 18.9 mwaka 2019, Sh bilioni 29 mwaka 2020 na Sh 88 bilioni kwa mwaka 2021.

Amesema Airtel Tanzania ilipaswa kuuza minara yake ambapo imeuzwa kwa dola milioni 175 na mununu ameshalipa milioni 157.

Amesema katika uuzaji huo Serikali itapokea Sh 43 bilioni na fedha zingine zitakwenda kuongeza uwekezaji na kulipa madeni, “kufikia Januari mwaka huu Airtel ilikuwa haina deni lolote linalodaiwa.”

Malata ambaye alishika wadhifa huo Januari 2020, amesema Airtel  imefanya biashara na kutekeleza maagizo ya wanahisa wote kama ilikuwa kwenye mkataba wa mwaka 2019.

Amesema ndani ya kipindi cha miaka mitatu kampuni hiyo imefanikiwa kuwa kampuni ya pili kwa umiliki katika soko la mawasiliano ya simu nchini ikiwa na wateja milioni 14.7.

Ameongeza kuwa imeweza kutoa ajira 350,000 kwa watanzania na kuendelea kutumia mkongo wa taifa kuboresha huduma zao.

Amesema imeweza kusambaza mtandao wa inteaneti wenye kasi ya 4G kote nchi na wamefikia asilimia 73 ya mradi wa kusambaza huduma hiyo.

Amesema pia wamefanikiwa kufungua maduka 2000 ya huduma za kifedha ambayo yanasaidia wananchi walio maeneo yasiyo na huduma za kibenki.

Aidha amesema wamechangia dola za Marekani milioni moja katika ujenzi wa Hospitali ya Uhuru iliyopo jijini Dodoma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Orb of Destiny kutoka Meridianbet kasino ushindi kwa njia 14  

Spread the love  ORB of Destiny ni mchezo wa sloti kutoka kwa...

Biashara

Jiandalie Strawberry Cocktail yako nyumbani huku unacheza kasino 

Spread the love  UTAANDAA matunda yako unayotaka kutumia unaweza kutumia Strawberry, Cantaloupe...

Biashara

420 Blaze It chimbo jipya la kuchota mihela Meridianbet kasino 

Spread the love  JE, umewahi kucheza mchezo wa droo wenye droo 10?...

Biashara

Exim yawainua kiuchumi wanawake wajasiriamali kupitia mpango wa WEP

Spread the love  BENKI ya Exim kupitia Mpango wake wa Kuwawezesha Kiuchumi...

error: Content is protected !!