Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari Simba yazindua kampeni ya hamasa kuimaliza Orlando
HabariMichezo

Simba yazindua kampeni ya hamasa kuimaliza Orlando

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba imezindua rasmi kampeni ya hamasa kuelekea mchezo wa hatua ya robo fainali wa michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, fdhidi ya Orlando Pirates ya nchini Afrika kusini. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa robo fainali ya kwanza utapigwa jumapili ya tarehe 17 Aprili 2022, kwenye dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam, majira ya saa 1 usiku.

Kampeni hiyo ya imezinduliwa leo tarehe 12 Aprili 2022, jijini Dar es Salaam eneo la Chang’ombe maduka mawili ili kutengeneza hamasa kwa mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye dimba la Benjamin Mkapa, kufuatia Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) kuwaruhusu Simba kuingiza Uwanjani mashabiki 60000.

Tukio hilo liliudhuliwa na viongozi mbalimbali wa klabu ya Simba, akiwemo Mwenyekiti wa klabu hiyo Murtaza Mangungu, Muhina Kaduguda mjumbe wa bodi ya wakurugenzi na Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo Mzee Hassan Dalali.

Akizungumza katika tukio hilo, Mwekekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu amesema kuwa katika mchezo huo wanakwenda kucheza mchezo huo ilikutafuta nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali, na hiulo linawezekana kwa sababu wanawachezaji wanaojitambua.

“Niwahakikishie Wanasimba na wapenzi wa soka, leo hii tunaenda kucheza mchezo kwa dakika 180 (nyumbani na ugenini) kutafuta nafasi ya kucheza nusu fainali sababu tuna wachezaji ambao wanajitambua, tuwaombee wafanye vizuri.” Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa Simba

Simba katika kipindi cha miaka mitano imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa barani Afrika mara mbili katika msimu tofauti.

Katika upande mwengine katibu mkuu wa zamani na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo, Muhina Seif Kaduguda alisema kuwa yupo tayari hata kufa ili Simba iweze kuwa bingwa wa michuano hiyo.

“Kama tumefanya kila kitu kuchukua ubingwa wa Afrika tumeshindwa na inatakiwa mtu afe, njooni mnichukue mimi nife Simba awe bingwa mimi nikawe kiongozi wa Semba ahela.” Alisema Kaduguda

Klabu hiyo itakuwa ni mara ya pili kukutana na timu kutoka Afrika Kusini katika hatua ya robo fainali, ambapo msimu uliopita Simba ilitupwa nje ya michuano hiyo na timu ya Kaizer Chief kwa jumla ya mabao 4-3.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!