March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Afya ya Dk. Kigwangalla yaimarika

Dk. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii (kulia) akizungimza na Naibu wake, Japhet Hasunga

Spread the love

HALI ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla inazidi kuimarika ambapo kwa mara ya kwanza tangu alazwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, amefanya mazoezi ya kupanda ngazi kwa miguu kutoka ghorofa ya kwanza hadi ya sita. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Waziri Kigwangalla alilazwa Muhimbili baada ya kupata ajali tarehe 4 Agosti mwaka huu, maeneo ya Magugu mkoani Manyara akiwa njiani akitokea Arusha kuelekea Dodoma.

Akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga aliyemtembelea hospitalini hap oleo tarehe 14 Agosti, 2018, Dk. Kigwangalla amesema hali yake inazidi kuimarika.

Awali, tarehe 12 Agosti mwaka huu, Dk. Kigwangalla alifanyiwa operesheni ya mkono na madaktari wa Muhimbili ambapo ilimalizika salama na sasa anaendelea vizuri.

error: Content is protected !!