Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Dereva wa mbunge auwawa na polisi
KimataifaTangulizi

Dereva wa mbunge auwawa na polisi

Spread the love

DEREVA wa Mbunge wa Jimbo la Kyaddondo Mashariki  nchini Uganda,  Robert Kyagulanyi  Bobi Wine, Yasin Kawuma amefariki baada ya kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa na polisi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Bobi Wine amedai kuwa dereva wake ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi akiwa ndani ya gari la mbunge huyo, wakidhani kuwa aliyekuwa kwenye gari ni yeye.

Mbunge huyo ambaye pia ni msanii wa muziki nchini humo, ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa walikuwa eneo linalojulikana kama Arua kwenye kampeni wakati mauaji hayo yalitokea.

Bobi Wine na viongozi kadhaa wa upinzani walikuwa eneo hilo kumuunga mkono mgombea huru Kassiano Wadri anayeshiriki katika uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya Mbunge wa jimbo hilo, Ibrahim Abiriga aliyeuawa.

Wakati wa kampeni hizo zikiendelea kulizuka vurugu kati ya wafuasi wa Wadri na wale wa mpinzani wake katika uchaguzi huo wa chama cha NRM, Tiperu Nusura.

Msemaji wa polisi Emilian Kayima, anasema watu waliokuwa wamevaa shati za kampeni za mgombea Wadri, walianza kuurushia mawe msafara wa rais hali ambayo ilisababisha polisi kufyatua risasi.

“Mwendo wa saa kumi na mbili jioni msafara wa rais ulishambuliwa na wahuni katika manispaa ya Arua wakati rais alikuwa anaondoka uwanja wa Boma ambapo alikuwa amefanya mkutano wa mwisho,” amesema Kayima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!