September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Afya ya Bwege yaimarika, aunganishwa na kina Zitto

Suleiman Bungara 'Bwege', aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF)

Spread the love

SELEMAN Bungara maarufu Bwege, Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) amefikishwa Kituo cha Polisi cha Lindi Mjini akitokea Kilwa Masoko. Anaripoti Faki Sosi, Lindi…(endelea).

Bwege ni miongoni mwa wanachama na viongozi sita wa chama cha ACT-Wazalendo waliokamatwa jana Jumanne asubuhi tarehe 23 Juni 2020 wakiwa katika kikao cha ndani kikiongozwa na Zitto Kabwe, Kiongozi wa chama hicho.

Walikamatwa wakidaiwa kufanya maandamano bila kibali. Kikao hicho kilikuwa kikyfanyikia ukumbi wa Starnford Bridge, Kilwa Masoko.

Baada ya kukamtwa, walipelekwa kituo cha Polisi Kilwa. Wakiwa hapo, hali ya afya ya Bwege ilibadilika na kuamua kupelekwa hospitalini ya Kilwa Masoko kwa matibabu na baadaye aliimarika na kurejeshwa tena kituoni hapo.

Wakati Bwege akiaendelea na matibabu, wenzake sita akiwemo Zitto walisafirishwa usiku wa kuamkia leo Jumatano kupelekwa Lindi mjini ambapo walifika saa 7:05 usiku.

Afya ya Bwege ambaye amekwisha kutangaza kujiunga na ACT- Wazalendo iliimarika nay eye kusafirishwa kutoka Kilwa hadi Lindi kuunga na wenzake ambapo amefikishwa asubuhi ya leo Jumatano.

Mbali na Zitto na Bwege, wengine ni Akida Mawanja, Mlinzi wa Zitto, Shaweji Mketo ambaye ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Swalehe Mketo aliyekuwa diwani wa CUF Kata ya Kibata, Abubakari Kama Mwenyekiti wa Jimbo Kilwa Kusini, Isihaka Mchinjika, Mwenyekiti wa Mkowa wa Lindi, na Mahadhi Mangona Katibu Mwenezi wa jimbo hilo.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

error: Content is protected !!