Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko THRDC, MISA-TAN yalaani kufutwa leseni Gazeti la Tanzania Daima
Habari Mchanganyiko

THRDC, MISA-TAN yalaani kufutwa leseni Gazeti la Tanzania Daima

Salome Kitomari, Mwenyekiti wa MISA-TAN
Spread the love

UAMUZI wa Idara ya Habari na Maelezo nchini Tanzania kusitisha leseni ya uzalishaji na uchapishaji wa Gazeti la Kila Siku la Tanzania Daima, umewaibua Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) kulaani kitendo hicho. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Jana Jumanne tarehe 23 Juni 2020, Idara ya Habari Maelezo, ilitangaza kusitisha  leseni ya uchapishaji na usambazji ya gazeti hilo linalomilikiwa na Kampuni ya Free Media Limited, kwa maelezo kwamba limekiuka masharti na sheria.

Akitangaza auamuzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Patrick Kipangula, alisema Tanzania Daima lilikiuka sheria na maadili ya uandishi wa habari kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Tanzania Daima halitakuwa mtaani kuanzia leo Jumatano tarehe 24 Juni 2020, hadi litakapoomba upya leseni au kukata rufaa kwa waziri mwenye dhamana ya habari.

Hatua hiyo imekosolewa na THRDC, huku MISA-TAN ikisema inafuatilia kwa ukaribu sakata hilo ili kutafuta suluhu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma jana Jumanne na MISA-TAN, taasisi hiyo ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika, imeahidi kufuatilia suala hilo.

“MISA Tanzania inafuatilia kwa ukaribu suala hilo na tutatoa taarifa kuhusu maendeleo ya ufuatiliaji huo,” inaeleza taarifa ya MISA-TAN.

Kwa upande wa THRDC, imelaani hatua hiyo ikidai kwamba, ni muendelezo wa ukiukwaji wa haki ya kikatiba ya uhuru wa kujieleza nchini Tanzania, kutokana na utekelezwaji wa Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya Mwaka 2016.

“Kusitishwa kwa uzalishaji na uchapishajiwa wa gzeti la Tanzania Daima ni muendelezo wa ukiukwaji wa haki ya uhuru wa kujieleza nchini Tanzania, uliotokana na utekelezwaji wa Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya Mwaka 2016,” inaeleza taarifa ya THRDC.

Onesmo Olengurumwa,Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu

“Tangu utekelezwaji wa sheria hiyo umeanza, tumeshuhudia magazeti kama Mawio, Mseto, MwanaHALISI, Rais Mwema, Mwananchi, The Citizen na Tanzania Daima, kufungwa kwa muda na mengine kusitishiwa leseni zao.”

THRDC imeiomba Serikali ya Tanzania kutekeleza uamuzi wa Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ), kuondoa  vifungu vya Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016, vinavyokinzana na misingi ya utawala bora, demokrasia na haki za binadamu.

Uamuzi huo umetokana na Kesi Na.2/2017 iliyofunguliwa mahakamani hapo na THRDC, kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania (MCT), na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC), kupinga vifungu kandamizi vya sheria hiyo.

“Tunaitaka Tanzania kuheshimu uamuzi wa Mahakama ya Afrika Mashariki wa kurekebisha sheria hiyo ili iendane na mkataba wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki (EAC),” inaeleza taarifa ya THRDC

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!