Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo watoa Mil 2 kuwachomoa Mbowe na wenzake
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo watoa Mil 2 kuwachomoa Mbowe na wenzake

Said Mohamed, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar
Spread the love

CHAMA cha ACT – Wazalendo kimechangia kiasi Sh. 2 milioni fedha taslim ili kuwezesha kutolewa gerezani viongozi wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliolala gerezani kusubiri kulipiwa faini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Fedha hizo zimekabidhiwa leo tarehe 11 Machi 2020, na kupokewa na Said Mohamed ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, anayekaimu nafasi ya mwenyekiti Freeman Mbowe.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya fedha hizo, Zitto Zuberi Kabwe, Kiongozi Mkuu wa chama, amesema kwa sasa vyama vya upinzani vinapaswa kuungana kuhakikisha kuwa viongozi hao wanakuwa huru.

“Tulisema tuje tuwaunge mkono kwa sababu hili si jambo lenu peke yenu, ni la kila Mtanzania, dhamana waliyoibeba si kwa ajili ya Chadema tu… bali kwa ajili ya demokrasia kulingana na mazingira ya sasa. Siwapi pole sababu wenyewe mashahidi mmeona kilichotokea,” amesema Zitto.

Zitto ameifananisha hukumu ya viongozi hao na hukumu aliyoipata Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kutokana na harakati zake za kudai uhuru wa Tanganyika.

Amesema Mwalimu Nyerere alipambana na mkoloni mweupe, lakini upinzani kwa sasa “unapambana na mkoloni mweusi.”

“Nyerere alipambana na mkoloni mweupe, sasa hivi sisi tunapambana na mkoloni mwenzetu mweusi CCM,” amesema Zitto

“Hatua hii ni mwanzo tu kwetu, tutaendelea kuchanga kuleta mchango na kutia moyo kwa wengine kuchanga mchango. Kisha tutaendelea kuratibu zoezi la uchangiaji.

Kaimu Mwenyekiti wa Chadema, Mohammed, ameshukuru uongozi na wanachama wa ACT-Wazalendo na kusema wameonesha upendo mkubwa.

“Niwashukuru sana uongozi wa ACT kwa ujumla. Mmekuwa pamoja nasi tangu mwanzo hata jana katika hukumu tulikuwa na viongozi wenu. Tulishirikiana vizuri na mkaonesha umoja tunaouhitaji katika kutafuta demokrasia na haki kushamiri,” amesema.

Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, amekishukuru na kupongeza chama hicho kwa mchango huo hususan katika kipindi hiki wenyewe mnahitaji fedha kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa viongozi.

“Tuwashukuru kwa dhati najua mnahitaji hela, hela mliyoitoa tunajua mko kwenye uchaguzi na uchaguzi wa chama unahitaji hela nyingi. Mmetoa sababu ya umoja na upendo. Haiwezekani hii hela kuwa ya ziada sababu mna mambo mengi. Tukiendelea kuwa hivi tutaweza kutoka hapa tulipo. Ni umoja wetu hatuna mjomba wala shangazi,” amesema Kigaila.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!