Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Faini Chadema: Mil 234 zachangwa
Habari za Siasa

Faini Chadema: Mil 234 zachangwa

Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimefanikiwa kukusanya Sh. 234 milioni, kwa ajili ya kulipa hukumu faini zaidi ya milioni 350, inayowakabili viongozi wake wakuu.  Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 11 Machi 2020, na Said Mohammed, Kaimu Mwenyekiti wa Chadema, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Mohammed amesema Sh. 176.9 milioni zilikusanywa kwa njia ya simu, Sh. 52.7 milioni zilikusanywa kwa njia ya benki na fedha taslimu milioni 4.7 zimepokelewa katika Ofisi za Makao Makuu ya Chadema.

Aidha, Mohammed ametoa wito kwa wafuasi wa Chadema na Watanzania kwa ujumla kuendelea kutoa michango, ili kupata fedha zilizobakia.

Amesema fedha hizo zilikusanywa kuanzia jana jioni hadi mchana wa leo tarehe 10 Machi 2020.

Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara, amesema fedha hizo zitatumika kuwatoa viongozi hao kwa mafungu.

Hata hivyo, Kigaila amesema faini waliyopigwa viongozi hao ni kubwa kuliko kosa walilotenda wahukumiwa hao.

“Uwiano wa faini na kifungo haulingani,  tunajua sababu. Wanajua hatuna fedha wakajua hawa watu wataoze agerezani. Niwashukuru Watanzania na WanaChadema. Tumeamua kuwatoa kwa mafungu. Tuendelee kuchanga ili tuwatoe wengine,” amesema Kigaila.

Viongozi waliohukumiwa ni, Freeman Mbowe, Mwenyekiti Chadema, John Mnyika, Katibu Mkuu Chadema, Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Bara, Halima Mdee, Mwenyekiti Bawacha.

Wengine ni Mchungaji Peter Msigwa, Mwenyekiti Chadema Kanda ya Nyasa, John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini na Esther Matiko, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti.

Hukumu ya faini ya Sh. 350 milioni au kifungo cha miezi mitano gerezani waliyohukumiwa viongozi hao, inatokana  na Kesi ya Uchochezi Na. 112/2018, iliyokuwa inawakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo,baada ya wahukumiwa hao kukutwa na hatia kwenye mashtaka 12 kati ya 13 yaliyokuwa yanawakabili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!