Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo waanika mapendekezo 7 kupata Tume Huru ya Uchaguzi
Habari za Siasa

ACT Wazalendo waanika mapendekezo 7 kupata Tume Huru ya Uchaguzi

Dorothy Semu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo Bara
Spread the love

 

Chama Cha ACT Wazalendo kimeutangaza mwaka wa 2022 kuwa mwaka wa kupigania Tume Huru ya Uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Pia chama hicho kimetoa mapendekezo saba yatakayowezesha kupatikana kwa Tume Huru ya Uchaguzi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu katika kikao na Viongozi wa ACT Wazalendo wa majimbo yote ya Mkoa wa Arusha kilichofanyika jijini humo leo tarehe 15 Januari 2022.

Amesema msimamo wa ACT Wazalendo upo bayana kwamba wanaanza na Tume Huru ya Uchaguzi ili kuweka mazingira ya kupata Katiba Mpya inayotokana na maoni na matakwa ya Wananchi.

“Sababu za kuhitaji Tume kwanza zipo wazi. Tunataka mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya usimamiwe na Tume ambayo ni huru.

“Pia, kwa kuzingatia ukweli kuwa mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya na kuanza kutumika unaweza kuhitaji muda zaidi, tunataka Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi,” amesema

Aidha, Dorothy ametaja mapendekezo saba ya ACT Wazalendo kuhusu utaratibu wa upatikanaji wa Tume Huru ya Uchaguzi.

Mojapoa ya mapendekezo hayo ni; Sheria mpya ya Uchaguzi (National Elections Act 2022) iweke utaratibu kuwa Watanzania wanaotaka kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi waombe kazi kufuatia tangazo la wazi kwa umma.

Pili; Sheria mpya ya Uchaguzi ianzishe Kamati Maalum ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.

Tatu; Kamati ya Uteuzi ifanye usaili kwa uwazi kwa waombaji wote na kuchuja majina ambayo yatapelekwa kwa Rais kwa ajili ya uteuzi.

Nne; Baada ya wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kupatikana wataajiri Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye nafasi itatangazwa, kufanyiwa usaili wa wazi na kisha jina kupelekwa kwa Rais kuteua Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Kiongozi huyo ametaja pendekezo la tano kuwa; Kamati ya Uteuzi wa Tume itamkwe kisheria kuongozwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kama Mwenyekiti, Jaji Mkuu wa Zanzibar kama Makamu wa Mwenyekiti, Wajumbe wawe ni Rais wa Tanganyika Law Society, Rais wa Zanzibar Law Society, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni,

“Mtu mmoja atakayeteuliwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na kama hakuna Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni basi kutoka chombo kinachojumuisha Vyama vyenye Wabunge Bungeni.

“Mtu mmoja kutoka Asasi ya Kitaifa ya masuala ya Sheria na Haki za Binaadam Tanzania Bara na mtu mmoja kutoka asasi kama hiyo Tanzania Zanzibar. Kwa vyovyote vile angalau theluthi ya wajumbe wa Kamati ya Uteuzi lazima wawe Wanawake,” amesema.

Sita; Kutakuwa na sifa maalum za Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha wanakuwa watu wenye weledi na hawaegemei upande wowote.

Saba; Baada ya kuteuliwa na Rais, Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume wataidhinishwa na Bunge kwa utaratibu utakaowekwa na Sheria ya Uchaguzi. Kisha watakula kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

Aidha, akizungumzia kuhusu Mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya, Dorothy amesema ACT Wazalendo inapendekeza Bunge kuunda Kamati ya Wataalam ili kutafuta namna bora ya kumalizia mchakato huo.

“Kwa sababu Katiba Pendekezwa haikutokana na maridhiano ya pande zote kutokana na wapinzani kususia hatua ya kupigia kura Katiba Pendekezwa kwenye Bunge la Katiba,” amesema.

Kaimu Mwenyekiti huyo anaendelea na ziara yake katika Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ambapo kesho tarehe 16 Januari 2022 atafanya kikao na viongozi wa Majimbo yote ya Mkoa wa Kilimanjaro kitachofanyika Moshi Mjini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!