January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanafunzi milioni 1.3 wafaulu kuendelea darasa la tano, hisabati donda ndugu

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde

Spread the love

 

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne ambapo takwimu zinaonesha kuwa jumla ya wanafunzi 1,347,554 kati ya wanafunzi 1,561,516 wenye matokeo ya Upimaji sawa na asilimia 86.30 wamepata ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kuendelea na Darasa la Tano. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Aidha, kati yao, wasichana ni 708,203 sawa na asilimia 87.65 na wavulana ni 639,351 sawa na asilimia 84.85.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo tarehe 15, 2022 na Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk. Charles Msonde yameonesha wanafunzi 213,962 sawa na silimia 13.70 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na Darasa la Tano.

Aidha, amesema wanafunzi wa Darasa la Nne 2021 wamefanya vizuri kwa masomo yote ambapo takwimu zinaonesha ufaulu wa chini ni asilimia 69.41 kwa somo la Hisabati na ufaulu wa juu ni 91.33 kwa somo la Maarifa ya Jamii kama ilivyoainishwa katika Jedwali la 2.

 

error: Content is protected !!