January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri wa mambo ya ndani kushiriki maombi ya kitaifa

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamadi Masauni

Spread the love

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni anatarajiwa kuongoza maombi maalumu ya kuliombea Taifa amani na utulivu yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumapili tarehe 16 Januari, 2022 katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage – Dodoma… (endelea)

Tukio hilo lililoandaliwa na Kanisa Halisi la Mungu Baba linatarajiwa kuwahusisha viongozi wa madhehebu mbalimbali nchini, viongozi wa serikali, wananchi pamoja na waumini wa dini zote kujumuika pamoja na kunyoosha vidole vyao kuombea amani ya taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 15 Januari, 2022 jijini Dodoma, Kuhani Moja Halisi kutoka Makao Makuu ya Kanisa hilo lililopo jijini Dar es Salaam, amesema wameandaa kusanyiko hilo ili kusaidia kuimarisha amani na mshikamano nchini.

Amesema jukumu la kanisa sio tu chini ya kuta nne, lakini kanisa linapaswa kutekeleza jukumu la kuunganisha na kutumikia jamii nzima na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, Kuhani Moja Halisi ameongeza kuwa kazi nyingine ya kila siku ya kanisa la kweli ni kumwomba Mungu ili viongozi wakuu wa kitaifa walindwe dhidi ya maadui, lakini pia waongozwe na Mungu katika utekelezaji wao wa kila siku.

“Amani na mshikamano ni miongoni mwa mambo muhimu ya kusukuma maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika taifa lolote lile, Watanzania wana kila sababu ya kumshukuru Mungu Baba kwa amani iliyopo,” amesema.

Aidha, Kuhani Ushindi Halisi amesisitiza umuhimu wa Watanzania kuhifadhi na kuendelea kuiombea nchi amani.

“Bila amani maendeleo ya kijamii na kiuchumi yanayohitajika sana nchini hayawezi kuona mwanga wa siku.

“Maendeleo yanataka amani na utangamano katika ngazi zote, kuanzia jumuiya za wenyeji, nchi jirani hadi ngazi za kimataifa, kwa sababu tunategemeana katika mchakato mzima wa uzalishaji, mnyororo wa ziada wa thamani pamoja na masoko,” amesema.

Kanisa Halisi la Mungu Baba ambalo linaongozwa na ‘Baba wa Uzao’ ina matawi yake katika nchi kadhaa ndani ya bara la Afrika, Ulaya na Amerika.

error: Content is protected !!