CHAMA cha siasa cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, kimesema kinakwenda kushiriki na kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge wa Muhambwe, mkoani Kigoma utakaofanyika tarehe 2 Mei 2021.
Uchaguzi huo, unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wake kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Atashasta Nditiye kufariki dunia tarehe 12 Februari 2021, kwa ajili ya gari, iliyotokea jijini Dodoma.
Fomu za kuomba kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zimeanza kutolewa kuanzia tarehe 28 Machi hadi 3 Aprili, kisha uteuzi utafanyika na kampeni kuanzia hadi 1 Mei 2021.
MwanaHALISI TV, limefanya mahojiano maalum na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo, ujumbe wao kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wananchi watarajie kampeni za aina gani.
Ado amegusia uchaguzi huu ambao ni wa kwanza kwa Rais Samia Suluhu Hassan kufanyika tangu alipoingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, wakimpa tahadhari ya kuchukua. Amejinasibu juu ya mgombea wao na yule wa Chama Cha Mapinduzi, Dk. Florence Samizi.
Fuatilia mahojiano yake na MwanaHALISI TV
Asante act kwa kuonesha matumain pasipo kuwa na matumain