September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo njia panda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman

Spread the love

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimedai kwamba Serikali ya Zanzibar, chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) , inakwenda kinyume na maridhiano yao ya kuanzisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK). Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Madai hayo yametolewa hivi karibuni na Mjumbe wa Kamati Kuu ya ACT-Wazalendo, Ismail Jussa, akihojiwa na Televisheni ya Zanzibar Kamili, visiwani humo.

“ACT-Wazalendo inaheshimu utawala bora na tumedhamiria kujenga jamii yenye maridhiano, ambayo imesimama katika misingi ya haki na amani. Tunachokiona kauli za ulaghai zinazotolewa kila siku,” amedai Jussa.

Jussa alidai “lakini inapokuja hasa wakati wa kuonesha vitendo tumeona watalawa na CCM rangi zao na tabia zao ni zilezile na hata akija nani, bado inaonekana kwao maslahi ya nchi si chochote, hiyo amani wanayoihubiri, haki wanayoihubiri si chochote, umoja wa wa Zanzibar si chochote.”

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya ACT-Wazalendo, alisema ACT-Wazalendo ina dhamira ya kuona Zanzibar inatulia kisisasa, lakini CCM haioneshi imani hiyo.

“Suala la imani sio la kuulizwa sisi, ni CCM wenyewe wanapaswa waonyeshe imani, sisi hatuna imani yao hawajaonyesha hiyo imani. Ni jukumu lao kuwaonesha watu kwamba kweli wana dhamira ya kuona Zanzibar inatulia,” alisema Jussa.

Jussa alimuomba Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi aheshimu maamuzi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Hayati Maalim Seif Shariff Hamad, ya kukubali kuunda SUK, ili kujenga umoja na mshikamano wa wananchi wa visiwa hivyo.

“ NimwambieRais Mwinyi, Zanzibar imetulia sababu aliyokuwa na imani na wa Zanzibar alishimka mkono na kuwataka wamuunge mkono, kuendelea kukalia kimya ayanayoendelea ni kupunguzia Wanzanzibar imani kwake,” alisema.

Miongoni mwa mambo yanayolalamikiwa na ACT-Wazalendo kwa Serikali ya Zanzibar, ni michakato ya chaguzi ndogo zilizofanyika visiwani humo, wakidai kuporwa ushindi na CCM katika chaguzi hizo.

“Katika hali ya kawaida kutokana na yaliyofanyika si Konde tu, ukitazama tulianza chaguzi ndogo ya Wadi ya Kinuni visiani Unguja, kuchagua diwani na Pandani Pemba, kulikuwa na uchaguzi mdogo wa uwakilishi lakini yaliyotokea ni yaleyale,’ alisema Jussa.

Leo Jumamosi, tarehe 31 Julai 2021, MwanaHALISI Online, ilimtafuta kwa simu Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Umma ACT-Wazalendo, Salim Biman, kuhusu msimamo wa ACT-Wazalendo juu ya malalamiko hayo.

Kaimu Naibu Katibu Mkuu ACT-Wazalendo-Zanzibar, Salim Bimani

Bimani ameueleza mtandao huu kuwa, Kamati Kuu ya ACT-Wazalendo, itakutana hivi karibuni visiwani Pemba, kwa ajili ya kujadili hali ya kisiasa Zanzibar.

“Kamati Kuu ya chama itakutana hivi karibuni visiwani Pemba, miongoni mwa mambo ambayo itazungumza ni hali ya uvunjifu wa amani, malalamiko ya chaguzi zilizofanyika katika Jimbo la Konde na maeneo mengine,” amesema Biman na kuongeza:

“Aliyosema Jussa ni kweli, kasema mengi ya ukweli, chaguzi zilizofanyika Pandani, Kinuni na Konde ndiyo ilikuwa na kasoro zaidi.”

MwanaHALISI Online imemtafuta Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka, kwa ajili ya ufafanuzi wa malalamiko hayo, ambaye hakujibu akisema chama chake kimeshatoa msimamo wake juu ya suala hilo.

Mapema Julai mwaka huu, Shaka alinukuliwa na vyombo vya habari, akiitaka ACT-Wazalendo iache chokochoko badala yake waache mshikamano na umoja wa wananchi wa Zanzibar, uendelee.

error: Content is protected !!