Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Abiria wamkunja nahodha MV Kigamboni
Habari za Siasa

Abiria wamkunja nahodha MV Kigamboni

Dk. Faustin Ndungulile, Mbunge wa Kigamboni
Spread the love

 

MBUNGE wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile amesema abiria wamelazimika kupigana na nahodha wa kivuko cha MV Kigamboni baada ya kusimamisha kivuko hicho kwa muda mrefu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ndugulile ameyasema hayo leo Jumanne tarehe 24 Mei, 2022 wakati akichangia hoja makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Mbunge huyo ambaye amewahi kuwa Waziri amesema usimamizi wa vivuko ni mbovu na TEMESA wameshindwa kazi yao, “kama wameshindwa kazi waseme ili vivuko vibinafsishwe.”

“Leo hii asubuhi nahodha wa MV Kigamboni amekunjwa na abiria wenye jazba kwasababu wamefika pale amewaweka kwa muda mrefu pale wakaamua kumfuata kule kule kwenye deck wameanza kupigana”

Ndungulile ametoa ushuhuda way eye mwenyewe kukwama kwenye kivuko kwa zaidi ya nusu saa kutokana na hitilafu.

Amesema hivi sasa inawachukua wananchi dakika 45 hadi saa zima kuvuka kutoka upande mmopja kwenda mwingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!