July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mayele atetema Mwanza, mabao 14 sawa na Mpole

Spread the love

BAO la dakika 74 lililowekwa kambani na Fiston Mayele kwenye mchezo dhidi ya Biashara United lilitosha kumfanya mshambuliaji huyo wa klabu ya Yanga kufikisha idadi ya mabao 14 kwenye Ligi sawa na George Mpole wa Geita Gold. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mayele alipachika bao hilo wakati Yanga ikilazimishwa sare mbele ya Biashara United na kuondoka na alama moja kwenye mchezo huo, na hivyo wanahitaji alama tatu kuwa bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Washambuliaji hao kwa sasa wapo kwenye Ligi ya peke yako katika kukitafuta kiatu cha ufungaji bora msimu huu wa 2021/22, huku wote wawili wakitumikia timu hizo kwa mara ya kwanza.

Mayele amepachika bao hilo, ikiwa imepita siku moja toka George Mpole alipofunga bao lake la 14 kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba uliopigwa kwenye dimba hilo hilo la CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Wawili hao huwenda wakafikia idadi ya mabao yaliyofungwa na mfungaji bora wa Ligi msimu uliomalizika John Bocco ambaye alipachika mabao 16.

Mpaka sasa kwa upande wa Mpole yeye pamoja na klabu yake ya Geita Gold wamebakisha jumla ya michezo mitano ili kutamatisha msimu huu sawa na dakika 450.

Vinara wa Ligi hiyo klabu ya Yanga mabo kwa sasa wanahitaji alama tatu kutangazwa kuwa mabingwa wapya, wao kwa upande wao wamebakisha michezo minne sawa na dakika 360.

error: Content is protected !!