MWANADIPLOMASIA kutoka nchini Urusi Borisi Bondarev, ameacha kazi kupinga vita vya umwagaji damu usiokuwa na msingi ulioanzishwa na Putin dhidi ya Ukraine. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).
Bondarev, ambaye alifanya kazi katiaka ubalozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa huko Geneva,aliiambia BBC kuwa alijua uamuzi wake huenda ukamaanisha kwamba Kremlin sasa inamwona kama msaliti.
Hata hivyo amesimama na kauli yake iliyoeleza vita hivyo kuwa ni ‘’uharibifu dhidi ya watu wa Ukraine ‘’na watu wa Urusi,” alisema.
Pia Moscow bado haijatoa tamko lolote kuhusu taarifa hiyo.
Urusi inakabiliana na wale wanaokosoa au kujiepusha na masimulizi rasmi kuhusu vita hivyo, ambayo inayataja tu kama “operesheni maalum ya kijeshi.’’
Aidha katika barua hiyo, iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii na kuwashirikisha wanadiplomasia wenzake,Bondarev ameeleza kuwa amechagua kukatisha maisha yake ya utumishi kwa miaka 20,kwasababu hangeweza kushiriki tena katika aibu hiyo ya umwagaji damu wa kipumbavu na usio namaana.
‘’Wale ambao wameanzisha vita hivi wanataka kitu kimoja tu kusalia madarakani milele .’’aliandika Bondarev.
Leave a comment