Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Biashara Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema
BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the love

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa kufanikiwa kukamilisha wa mchakato wa ununuzi wa hisa za Kampuni ya Ore Corp na kuitaka kampuni hiyo kukamilisha haraka malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha mradi wa uchimbaji dhahabu wilayani Sengerema mkoani Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mavunde amebainisha hayo leo tarehe 19 Aprili alipofanya kikao cha pamoja na Kampuni ya Perseus ya Australia ikiongozwa na Mtendaji Mkuu wake, Jaffer Quartamaine.

Kikao hicho kilizungumzia uendelezwaji wa mradi wa Nyanzaga unaomilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Ore Corp ambayo hisa zake zimenunuliwa na Kampuni ya Perseus.

Pia amewataka wawekezaji hao kuhakikisha wanaanza mapema uendelezaji wa mradi kwa mujibu ya makubaliano ya awali ya kimkataba ili nchi ianze kunufaika na matunda ya utekelezaji wa mradi wa uchimbaji mkubwa wa madini dhahabu wa Nyanzaga uliopo Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Akizungumza katika kikao hicho, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Perseus, Jaffer Quartamaine ameishukuru serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa wakati wote wa mchakato wa ununuzi wa hisa za Kampuni ya Ore Corp.

Pia  ameahidi kwamba wamejipanga kuanza uendelezaji wa mradi huu mapema kadri iwezekanavyo kutokana na mpangilio wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za utekelezaji wa mradi.

Ameongeza pia kwamba wamejipanga kufanya uwekezaji mkubwa na wa mfano kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuongeza uzalishaji wa dhahabu nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Meridianbet watoa msaada wa chakula Chamazi

Spread the love  JUMAMOSI ya leo Meridianbet wametua pale Chamazi Magengeni kwaajili...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB ‘yafunga ndoa’ na wanawake wanaomiliki shule, vyuo Tanzania

Spread the loveBENKI ya NMB imeingia makubaliano rasmi (MoU) na Chama cha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!