Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makonda kuanika mawaziri wanaomtukana Samia
Habari za SiasaTangulizi

Makonda kuanika mawaziri wanaomtukana Samia

Spread the love

MKUU Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewataka watu wanaowatuma mawakala wao kumtukana mitandaoni Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, waache mara moja kwani wasipofanya hivyo atawaanika hadharani kwa kuwa ana majina yao wakiwemo mawaziri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza katika kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, hayati Edward Sokoine, leo Ijumaa jijini Arusha, Makonda amedai kuna watu wenye lengo la kumkatisha tamaa Rais Samia, hivyo anamuomba Mungu ampe ulinzi wa moyo wake ili aendelee kuwatumikia watanzania.

“Nakuombea kwa Mungu akupe wigo wa bullet proof itakayolinda moyo wako ututumikie sisi watanzania, nafahamu wenye maneno na hawaishi kusema maneno lengo lao ni kukukatisha tamaa tena wengine umetupa nafasi tumo ndani ya uongozi wako na nitumie fursa hii kuwaambia hasa kaka zangu mnaotuma na kulipa watu kumchokoza mama yangu Samia, mnanijua na ninyi nawajua,” amesema Makonda.

Makonda amesema “kwa majina yao nawajua na leo tarehe 12 nataka iwe mwisho kuwatuma watu hao wanaotukana kwenye mitandao ya kijamii. Ikiendelea Jumatatu nakutajia majina wengine mawaziri na wengine wanapewa nguvu na watu tunaowaheshimu, naomba iwe msiho tumuache afanye kazi aliyopewa na Mungu.”

Katika hatua nyingine, Makonda amemshukuru Kardinali Polycarp Pengo kwa kuwa naye karibu katika nyakati zote alipokuwa na cheo na hata alipokuwa hana cheo.

“Nitambue nafasi ya baba wangu na mlezi wangu wa kiroho Kardinali Pengo, mzee huyu ni wa tofauti sana nimekuwa naye kwa nyakati zote nilizopitia, nilipokuwa na cheo alikuwepo nilipokuwa sina cheo alikuwepo. Kwa hiyo ninapomuona amefika mahala hapa naiona heshima na upendeleo wa kimungu kukanyaga kwenye ardhi uliyonipa kuiongoza, ardhi haitazaa tena mapooza,” amesema Makonda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!