Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Ridhiwani Kikwete amesema katika mwaka huu wa fedha unaoishia 2023/2024, Serikali imepanga kupandisha madaraja kwa mserereko walimu 52,551. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya walimu hao kutimiza vigezo kwa mujibu wa uchambuzi na uhakiki ambao umekamilika.
Kikwete ametoa kauli hiyo leo Jumatano bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Ngara, Ndaisaba Ruhuro (CCM) aliyehoji mpango wa wa kupandisha madaraja msrereko walimu wenye changamoto ya kupandishwa madaraja wakiwemo wa Ngara.
Akijibu swali hilo, Kikwete amesema kwa upande wa Halmashauri ya Ngara, walimu 148 ambao wametimiza vigeo watapandishwa.
Na Mimi ni miongoni mwa wahanga wa changamoto hiyo , ebu tusubili tuone Kam mungu atatujalia tupande
Nampongeza mama na Raise Samia kwa namna anavyotujali wafanyakazi.Deni letu kwake ni kufanya kazi kwa bidii na weredi.
Let it be yes and not politics as usual,just imagine it’s almost ten years of poor promotions and salary increase after the retire of president JAKAYA MRISHO KIKWETE he was the hope of workers for sure .May PRESIDENT SAMIA SULUHU HASAN follow his steps back ,I’m sure she will ,as she has started to work upon many workers problems that has made them workers to suffer a lot .
Baodo sijamwamini mana alishatudanganya
Ni ikitokea