Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Jela miaka 25 kwa kukutwa na kilo 107.29 za bangi
Habari Mchanganyiko

Jela miaka 25 kwa kukutwa na kilo 107.29 za bangi

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, kanda ya Morogoro imemhukumu miaka 25 jela John Mwaseba Mwasikili baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye ujazo wa kilo 107.29. Anaripoti Yusuph Kayanda, Morogoro … (endelea).

Akitoa hukumu hiyo Jaji wa mahakama hiyo, M. P.Otaru amesema ushahidi uliotolewa na mashahidi 16 na vielelezo 15 vya upande wa mashitaka haukuacha shaka dhidi ya mshitakiwa kutenda kosa hilo.

Jaji Otaru amesema kuwa amemtia hatiani mshtakiwa huyo baada ya kujiridhisha kuwa ni kweli mshitakiwa alikamatwa na dawa ya kulevya aina ya bangi yenye uzito wa kilogram 107.29 iliyokuwa ndani ya gari aina ya Toyota Kluger namba T.895 CQR kwenye mifuko nane ya sulphate.

Mahakama pia imeamuru gari namba T 895 CQR ambalo lilikuwa na bangi hiyo litaifishwe na kielelezo ambacho ni dawa za kulevya aina ya bangi kuteketezwa.

Mshitakiwa Mwasikili alikamatwa na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya na kufikisha katika Mahakama kuu kanda ya Morogoro Machi 15, 2024.

Inadaiwa kuwa mwaka 2022 huko Morogoro lilikamatwa gari aina ya Toyota Kluger lenye namba za usajili T.985 ambalo ndani yake lilikutwa na mifuko nane ya sulphate ikiwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile aukwaa uenyekiti wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!