Monday , 13 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Babu Duni atema bungo ACT-Wazalendo
Habari za Siasa

Babu Duni atema bungo ACT-Wazalendo

Spread the love

BAADA ya kuibuka tetesi za kwamba Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Chama cha ACT-Wazalendo Taifa, Babu Juma Duni Haji, anashinikizwa asitetee tena kiti hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika wiki hii, sasa mwanasiasa huyo amejiondoa rasmi katika mbio hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Leo tarehe 4 Machi 2024, ikiwa imesalia takribani siku moja kwa uchaguzi wa nafasi hiyo kufanyika, Babu Duni, ameiomba Halmashauri Kuu ya ACT-Wazalendo ajiondoe katika kinyang’anyiro hicho huku akitaja sababu saba zilizopelekea achukue uamuzi huo. Ombi hilo lilikubaliwa.

“..Leo nimekabidhi rasmi barua yangu, kuhusu kuondoa nia (kujitoa) kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama taifa. Nimechukua uamuzi huo kwa mujibu wa Katiba ya Chama Ibara ya 11(3)(7) na Ibara ya 76(1)(p) na Ibara ya 111(3) zikisomwa pamoja, juu ya haki ya kuchagua na kuchaguliwa.

“Hivyo napenda kuchukua fursa hii kuwaomba viongozi wenzangu na Wajumbe wa Halmashauri Kuu kuridhia kujitoa kwangu katika mchakato wa kugombea nafasi hiyo na kutopoteza muda wenu kutekeleza takwa la Katiba Ibara tajwa hapo juu,” Babu Duni aliwaeleza wajumbe wa halmashauri hiyo wakati anawasilisha kusudio lake la kujitoa.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa na Babu Duni kwamba zimepelekea kujitoa kwenye uchaguzi huo ambao alikuwa anachuana na Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar anayemaliza muda wake, Othman Masoud Othman, ni kuzingatia maslahi mapana ya chama hicho.

Babu Duni amesema ameamua kujiweka kando ili Othman akabidhiwe nafasi hiyo kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kudai haki.

Sababu nyingine ni, kuzingatia ushauri, maoni au mapendekezo ya viongozi wenzake, kuimarisha umoja na maelewano miongoni mwao, kuelekeza nguvu zao dhidi ya washindani wa kisiasa wa ACT-Wazalendo na kuepusha migawanyiko.

Msimamo huo wa Babu Duni ameutoa ikiwa zimepita siku kadhaa tangu atamke hadharani kwamba hayuko tayari kujitoa katika nafasi hiyo, huku akituhumu baadhi ya watu kumtengenezea hujuma ili asichaguliwe tena.

“Kauli yangu ni moja tu, tushikamane tujenge chama chetu tushinde viti vingi vya udiwani, wabunge na huku wawakilishi. Suala la kutaka kujenga mfarakano hatufiki mbali na hao wanaokuwa na hofu ya kupoteza vyeo vyao tukishafarakana na vyeo vya havipo na mimi hata nipate kura moja kwenye mkutano mkuu itakuwa ni kura ya kwamba mimi najitambua na najiamini,” alisema Babu Duni kabla hajajitoa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Msukuma aibana Serikali ujenzi nyumba za watumishi Geita DC

Spread the loveMBUNGE wa Geita, Joseph Msukuma (CCM) ameishauri Serikali kutenga bajeti...

AfyaHabari za Siasa

Vifo vitokanavyo na UKIMWI vyapungua

Spread the loveVIFO vinavyosababishwa na Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI), vimepungua kutoka...

AfyaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

NBC yazindua kadi uanachama msalaba mwekundu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!