Sunday , 12 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: Mwinyi chanzo cha mageuzi
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Mwinyi chanzo cha mageuzi

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia, Freeman Mbowe amesema huwezi kuliacha jina la Ally Hassan Mwinyi unapotaja mageuzi nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, Mbowe amesema wakati Mzee Mwinyi anaingia madarakani kama Rais wa awamu ya Pili mwaka 1985, alipokea nchi ambayo ilikua na changamoto lukuki.

“Tanzania kwa kipindi kile ilikua katika harakati za kutafuta namna bora zaidi ya kusonga mbele baada ya kipindi cha ujamaa.

“Miaka ya urais wake iliyompa jina la utani la Mzee Rukhsa ilikua msingi wa ujenzi wa taifa lenye dira na muelekeo mpya.  Rais Mwinyi atakumbukwa sio tu kwa vyeo na uraisi bali pia uwajibikaji, na ubinadamu wake.

“Taifa limepoteza kisima cha busara na nembo muhimu. Natoa pole zangu dhati kwa familia, ndugu, jamaa na taifa kwa msiba huu mzito.  Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un,” ameandika Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!