Tuesday , 14 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia
Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Sugu
Spread the love

ALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano na mkutano wa hadhara wa chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kufikisha ujumbe kwa mrithi wake, Spika Tulia Ackson. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Tukio hilo limetokea leo tarehe 20 Februari 2024, jijini Mbeya baada ya Sugu kutumia mkutano huo kujaribu kuonesha kuwa Spika Tulia ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini, hakubaliki kwa wapiga kura wake.

Ni baada ya kuwahoji wangapi hawakumchagua Spika Tulia, hawakumjibu lakini alipowauliza wangapi walimchagua katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, wengi waliinua mkono na kuitika kwamba walimchagua.

“Hapa mmeonyesha wazi kabisa kwa sababu hizi ni kura, wangapi hawakumchagua Tulia hapa? Wangapi mlimchagua Sugu akaporwa mikono juu. Tutaendelea kuandamana maisha magumu, chakula bei ghali, petrol bei ghali,” amesema Sugu.

Naye Boniface Mwabukusi aliwataka wananchi wa Mbeya Mjini wasimchague Spika Tulia kwa madai kuwa alishiriki kupitisha mkataba wa uwekezaji bandarini aliodai ulikuwa hauna maslahi kwa taifa.

“Kazi yetu moja ya kuwafurahisha watanzania, ni kuhakikisha sio tu kukaribia bungeni bali anapiga picha akiwa kilomita 1,200 akiwa hapa asirudi tena,” alisema Mwabukusi.

Tangu Bunge lipitishe azimio la kubariki mkataba huo, baadhi ya wanasiasa walimvaa Spika Tulia kwa madai kuwa amekubali lipitishe mkataba mbovu. Hata hivyo, kiongozi huyo wa Bunge pamoja na wabunge wake walijitetea kwamba wameupitisha baada ya kujiridhisha hauna shida kisheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Madeleka aibwaga Jamhuri kesi za kubambikiwa

Spread the loveWakili Peter Madeleka ameshinda rufaa yake namba 263 ya mwaka...

Habari za SiasaTangulizi

Sheikh Ponda ataka kura ya maoni kuamua hatma ya muungano

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

Habari za Siasa

Bunge lakemea utoroshwaji mifugo kuelekea Kenya

Spread the loveKamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na...

Habari za Siasa

CUF yajipanga kuelekea chaguzi zijazo

Spread the loveCHAMA cha Wananchi (CUF), kimejipanga kujijenga kisiasa kuelekea chaguzi zijazo...

error: Content is protected !!