Monday , 13 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Selasini: CCM walitunyima vingi kumzuia Lowassa kugombea urais
Habari za Siasa

Selasini: CCM walitunyima vingi kumzuia Lowassa kugombea urais

Joseph Selasini, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya NCCR Mageuzi
Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini, amedai Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewafanya watanzania kutonufaika na Hayati Edward Lowassa, kufuatia hatua yake ya kumkwamisha kwenye harakati zake za kugombea Urais wa Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).

Selasini ametoa kauli hiyo akizungumzia mapito ya kisiasa ya Lowassa, aliyefariki dunia tarehe 10 Februari 2024, akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam, kisha mwili wake kuzikwa Jumamosi iliyopita nyumbani kwake Monduli, mkoani Arusha.

Mbio za Lowassa kugombea urais wa Tanzania kupitia CCM zilikoma 2015, baada ya jina lake kukatwa katika Mkutano Mkuu wa chama hicho.

“Tuanze kujilaumu kwa kumchanganya akaacha uwaziri mkuu na naamini angemaliza miaka mitano ya uwaziri mkuu kungekuwa na mabadiliko makubwa sana, hilo ni la kwanza.

“La pili tuache siasa za kuibiana kura ndani ya vyama vyetu tuchague watu kwa haki na tuwaache wapiga kura wachague. Lazima tujilaumu kwa kumkosa Lowassa sababu alikuwa na ushauwishi mkubwa kwenye mkutano mkuu wa CCM 2015 na bado akakatwa licha ya wajumbe wengi kumtaka,” alisema Selasini.

Selasini alisema “huo ubabe ndiyo unatunyima viongozi na tunajilaumu kwa sababu tunaacha viongozi wanaopendwa na watu ambao wako tayari kushirikiana nao tunaweka viongozi kwa sababu tunazotaka sisi. Kama angekuwa rais tungenufaika na uthubutu wake katika kufanya maamuzi, yako mambo mengi sana ambayo yanahitaji watu kuthubutu na yanakwenda.”

Katika hatua nyingine, Selasini alisema Lowassa amegoma kufa, kwa kuwa hata baada ya umauti wake kumfika lakini bado yupo midomoni mwa watanzania, kitu ambacho ni nadra kutokea.

“Nimeona kwa mara ya kwanza mtu aliyekufa lakini akakataa kufa. Lowassa kafa lakini amekataa kufa, unajua maana yake? Kila mtu anamzungumzia kama yupo hapa sasa hivi maana yake kazi zako utakazofanya duniani ndizo zitakazokufanya uishi na sio umili wako wa pesa, mali na utajiri mwingi,” alisema Selasini.

Alisema Hayati Lowassa aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, alikuwa mtulivu kwani kama asingekuwa mtulivu angesababisha machafuko kama angetumia nguvu ya umma kupinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa CCM, Hayati Dk. John Magufuli.

“Kwa siasa hizi za visasi na za ajabu za nchi yetu, lakini Lowassa alikuwa mtulivu. Kwa umati aliokuwa nao nchi nzima angeamua kisasi, lakini hakuwa mtu wa kisasi aliona basi hata hili niache. Lengo lake kubwa ilikuwa kuonyesha nina wafuasi wa kutosha aliounesha kwenye uchaguzi, watu walikuwa wanatembea na wasanii lakini yeye alikuwa peke yake na watu waliokuwa wengi,” alisema Selasini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wizara kutumia Sh. 3.5 bilioni kuchunguza afya ya akili, nguvu za kiume

Spread the loveWIZARA ya Afya, imepanga kutumia Sh. 3.50 bilioni, kwa ajili...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC yapaza sauti changamoto ya intaneti

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umeitaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Prof. Ndakidemi aitaka TMA kutoa taarifa kwa njia ya SMS

Spread the loveMBUNGE wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi (CCM) ameishauri Serikali...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Msukuma aibana Serikali ujenzi nyumba za watumishi Geita DC

Spread the loveMBUNGE wa Geita, Joseph Msukuma (CCM) ameishauri Serikali kutenga bajeti...

error: Content is protected !!