Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mwigulu: Ushirikiano mzuri umestawisha sekta ya madini Tz
Habari Mchanganyiko

Dk. Mwigulu: Ushirikiano mzuri umestawisha sekta ya madini Tz

Spread the love

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amesema mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Serikali na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) yamechangia kukuza uchumi wa Taifa hususan kwenye makusanyo mazuri ya kodi, ajira na manunuzi ya bidhaa na huduma kutoka ndani ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Pia amesema GGML ambao wamekuwa wadau wazuri kwenye sekta ya madini pamoja na ushirikiano mzuri unaotolewa kwa wizara ya madini umeendelea kukuza sekta hiyo ya madini na kutoa mchango mkubwa kwa jamii na Taifa.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba (kulia), akisalimiana na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya AngloGold Ashanti (AGA), Gillian Doran (kushoto) aliyemtebelea ofisini kwake wiki iliyopita. Anayefuata kushoto ni Makamu Rais wa AngloGold Ashanti -GGML anayeshughulikia miradi endelevu na masuala ya ubia/ushirika (Afrika), Simon Shayo pamoja na viongozi wengine wa GGML. Wakati wanaofuata kulia ni baadhi ya maofisa wa wizara ya fedha.

Dk. Mwigulu ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dodoma alipokuwa anazungumza na Afisa Mkuu wa masuala ya Fedha wa Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Anglo Gold Ashanti, inayomiliki mgodi huo wa Geita Gold Mine-GGM), Gillian Doran.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Mwigulu alisema; “Tumekuwa na mahusiano mazuri sana na GGML kama wizara ya fedha hususani katika masuala ya kikodi na kiuchumi.

“GGML wamekuwa wadau muhimu sana wa masuala ya kodi na masuala ya kukuza uchumi wa nchi yetu pia wamekuwa mahusiano mazuri na wizara ya kisekta (madini) kwa kuwa moja ya mgodi wa mfano ambao una ushirikiano mkubwa na wizara ya kisekta na wizara nyingine kama sisi,” alisema Dk. Mwigulu.

Aidha, alisema GGML umekuwa moja ya mgodi wa mfano wenye mahusiano mazuri na jamii mgodi ulipo kwa kutekeleza ipasavyo mpango wa uwajibika wa kampuni kwa jamii (CSR).

Pamoja na mambo mambo mengine alitoa wito kwa kampuni hiyo kutumia viwanda vya kuchenjua dhahabu kwa njia ya kusafisha iliyopo nchini ili kuendelea kukuza uchumi wa Taifa.

Aidha, katika majadiliano hayo Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya AngloGold Ashanti (AGA), Gillian Doran aliyemtembelea Dk. Mwigulu akiwa na timu ya uongozi wa kampuni hiyo, alimweleza waziri huyo kuhusu mipango ya muda mrefu ya AngloGold Ashanti kwa Tanzania.
Alimshukuru Dk. Mwigulu kwa kutambua mchango wa GGML ambayo imeendelea kusalia kuwa mlipakodi bora zaidi katika tasnia ya uziduaji nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!