Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Shule za serikali zang’ara matokeo kidato cha nne, 102 wafutiwa matokeo
Habari MchanganyikoTangulizi

Shule za serikali zang’ara matokeo kidato cha nne, 102 wafutiwa matokeo

Spread the love

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika Novemba 2023, ambapo watahiniwa 484,823 (87.65%) wamefaulu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akitangaza matokeo hayo, leo tarehe 25 Januari 2024, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Said Ally Mohamed, amesema watahiniwa wa kike wamefaulu wengi zaidi wakati wakiume wakifaulu vizuri.

“Ufaulu kwa ujumla umepanda ukiangalia asilimia zaidi ya 87 ya waliofaulu wametoka kwenye shule za Serikali, asilimia 13 kutoka shule binafsi,” amesema Dk. Mohamed.

Amesema katika mtihani wa 2023, kumekuwa na ongezeko la shule zilizopata wastani wa daraja la A mpaka D na A mpaka C ikilinganishwa na 2022. Ufaulu asomo ya sayansi ya jamii (Historia, Jiographia na Uraia), umeongezeka huku Kiswahili kikiongoza kwa kuwa na ufaulu wa asilimia 96.8 katika alama A.

Somo la hisabati nalo ufaulu wake umeongezeka kwa asilimia 5.4 kutoka asilimia 20.08 mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 25.08 mwaka 2023.

Katika hatua nyingine, Dk. Mohamed amesema watahiniwa 102 wamefutiwa matokeo kwa makosa ya udanganyifu na kuandika matusi, huku 376 matokeo yao yakizuiliwa baada ya kupata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani.

“Wapo watahiniwa wamesaidiana humo ndani wamekamatwa, lakini ipo kesi moja mwalimu mkuu amesaidia watahiniwa wake hilo litafanyiwa kazi kwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu,” amesema Dk. Mohamed.

Kuangalia matokeo yote ya kitado cha nne ingia hapa

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!