Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mafuriko yatikisa Kongwa, DC afunguka
Habari Mchanganyiko

Mafuriko yatikisa Kongwa, DC afunguka

Spread the love

MAFURIKO ya maji  mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya wilayani Kiteto mkoani Manyara, yamesababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara ya Morogoro-Dodoma, baada ya kufunga eneo la Kongwa mkoani Dodoma kwa saa kadhaa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu, leo tarehe 9 Januari 2024, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mayeka Simon Mayeka amesema mafuriko hayo yalisababisha maji kujaa katika barabara eneo la Kongwa, na kusababisha magari na raia kushindwa kuitumia.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mayeka Simon Mayeka.

Mayeka amesema kwa sasa maji hayo yamepungua na kwamba magari yameanza kuruhusiwa kutembea kwa awamu, huku akitaja athari za mafuriko hayo kuwa ni gari moja lililolazimisha kupita kabla ya kuruhusiwa na kudondoka. Hata hivyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa au kupoteza maisha kufuatia mafuriko hayo.

“Ni sahihi kulikuwa na hali mbaya ya mafuriko toka asubuhi lakini sasa maji yameshapungua na tumeanza kuruhusu magari machache yapite kwa awamu. Athari kwa maana ya binadamu kupoteza maisha hakuna ila kuna gari lilijaribu kupita kabla ya askari kuruhusu lilidondoka,” amesema Mayeka na kuongeza:

“Chanzo cha mafuriko haya ni maji tunayopokea kutoka wilayani Kiteto ambako kunanyesha mvua sababu sisi huku mvua haikunyesha na sababu Kongwa iko chini maji yanajaa.”

Kuibuka wa taarifa hizi kumekuja baada ya baadhi ya wananchi kusambaza video zinazoonyesha barabara hiyo kujaa maji huku magari yakiwa kwenye mlolongo wa foleni baada ya kukwama kupita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile aukwaa uenyekiti wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!