Afisa mkuu wa Vatican ambaye pia ni mshauri wa Papa Francis, Askofu Mkuu Charles Scicluna amesema ipo haja ya Kanisa Katoliki kutathmini upya suala la mapdre kuoa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Charles Scicluna ambaye ni Askofu Mkuu wa Malta ametoa ushauri huo katika mahojiano yaliyochapishwa jana Jumapili na gazeti la Times of Malta.
Alisema: “Ni mara ya kwanza ninayasema haya hadharani na huenda yataonekana kuwa ya uzushi kwa baadhi ya watu.”
Askofu Scicluna, anayejulikana zaidi kwa uchunguzi wake wa uhalifu wa unyanyasaji wa kijinsia, alibainisha kuwa makasisi waliruhusiwa kuoa katika milenia ya kwanza ya historia ya Kanisa na kwamba ndoa inaruhusiwa leo katika ibada ya Mashariki ya Kanisa Katoliki.
“Kama ningelikuwa na uwezo, ningerekebisha masharti ya kuwataka makasisi kuwa waseja,” alisema na kuongeza kuwa;
“Uzoefu umenionyesha kuwa hili ni jambo tunalohitaji kufikiriwa kwa uzito.”
Askofu Mkuu Scicluna, 64, alisema Kanisa “limepoteza makasisi wengi wakuu kwa sababu walichagua ndoa”.
Alisema kuna mahali kwa useja katika Kanisa lakini pia ilibidi kuzingatia kwamba kasisi wakati mwingine wanapata hisia ya mapenzi.
“Hilo linapotokea anapaswa kuchagua kati ndoa na ukuhani na baadhi ya makuhani katika juhudi za kukabiliana na uamuzi huo wanaingia kisiri katika mahusiano ya kimapenzi”.
Mjadala kuhusu iwapo makasisi wa Kikatoliki waruhusiwe kuoa umekuwepo kwa karne nyingi.
Leave a comment