Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Hospitali ya Kairuki yaleta neema wanawake wasiopata watoto
Habari Mchanganyiko

Hospitali ya Kairuki yaleta neema wanawake wasiopata watoto

Spread the love

JITIHADA zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kuigeuza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba zinaendelea kupata mafanikio makubwa baada ya ya Hospitali ya Kairuki ya Mikocheni jijini Dar es Salaam kuanza kutoa matibabu ya kuondoa vimbe mbalimbali bila upasuaji kwa  kutumia mtambo tiba unotumia mwangwi wa sauti (Ultrasound). Anaripoti Mwandishi Wetu….(endelea)

Rais Samia amekuwa akifanya jitihada kubwa kuzipa vifaa hospitali za serikali na kuziwekea mazingira rafiki hospitali binafsi ili ziweze kununua vifaa tiba vya kisasa na kutoa tiba za kibingwa ambazo awali wagonjwa walilazimika kuzifuata Ulaya, Marekani na India.

Mtambo mpya na wa kisasa ambao umenunuliwa na Hospitali ya Kairuki  unaoitwa High Intensity Focused Ultrasound (HIFU), umeelezwa kuwa mkombozi mkubwa kwa watu waliokuwa na matatizo ya uvimbe hawa wanawake ambao wamekuwa wakipata changamoto ya uzazi.

Mtaalamu mwendeshaji wa mtambo huo, Dr. Fredy Rutachunzibwa, alisema mtambo huo tiba unatibu vimbe za aina mbalimbali kwenye kizazi, figo kongosho, ini, mifupa, matiti na uvimbe wowote unaoweza kuonekana kwenye mtambo huo.

Wataalamu wakimwandaa mgonjwa kuingiza kwenye mtambo mpya na wa kisasa ambao umenunuliwa na Hospitali ya Kairuki unaoitwa High Intensity Focused Ultrasound (HIFU), ambao unatibu uvimbe bila upasuaji kwa kutumia mwangwi wa sauti.

“Tunamshukuru sana Rais wetu kwasababu haya yote ni mafanikio ambayo yametokana na jitihada zake za kuigeuza Tanzania kuwa kituo cha utalii tiba,  tiba kama hii si kwamba itawanufaisha watanzania pekee tunatarajia wagonjwa wengi Afrika watamiminika kupata tiba hii Tanzania kwasababu hii ni teknolojia mpya,” alisema

Alisema kuwa mtambo huo ambao ulianza kufanyakazi Januari mwaka huu, unao uwezo wa kutibu hadi wagonjwa 10 kwa siku.

Alisema faida za tiba kwa kutumia mtambo huo ni kwamba mgonjwa hapati maumivu makali,  anapata nafuu haraka, kutopoteza damu na kuepukana na makovu ya upasuaji.

Alisema tayari wagonjwa wanne (4) wamefanyiwa matibabu hayo tangu kuwasili kwa  mtambo huo ambao unatarajiwa kuzinduliwa rasmi hivi karibuni.

“Mtambo huu mbali na kuwa na uwezo huo utawanufaisha sana wanawake wenye kusumbuliwa na vimbe zinazosababisha changamoto za uzazi sasa vimbe zikiondolewa watapata ujauzito kwa urahisi,” alisema

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki, Dk. Asser Mchomvu, alisema mtambo huo ni wanne (4) kwa Afrika na kwamba uko pia kwenye nchi za Misri, Afrika Kusini, Nigeria na sasa uko Tanzania kwenye hospitali hiyo.

Alisema hospitali hiyo imewapeleka nje ya nchi wataalamu wake wawili kupata mafunzo na tayari wamemaliza na wameshabobea kuendesha mtambo  huo.

“Uwezo wa mashine ni kutibu hadi wagonjwa 10 kwa siku ila inategemea aina ya vimbe aliyonayo mgonjwa.  Kwasababu kuna mwingine anakuwa na vimbe hata nne,” alisema na kuongeza

“Zamani tulikuwa tunafanya upasuaji kwa kufungua tumbo, tukahamia kwenye njia ya upasuaji kwa kutumia matobo na sasa hivi tumeendelea zaidi tunatoa uvimbe huo huo bila kupasua wala kuweka matobo hiki nikiwango cha juu zaidi cha matibabu,” alisema

Dk. Mchomvu alisema tayari Hospitali hiyo imeunda timu maaalum ya kutibu bila kufanya upasuaji inayoitwa HIFU Kliniki itakayokuwa inaendeshwa na wataalamu wabobezi wa hospitali hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!