Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Semesi ateuliwa kuwa mkurugenzi mpya NEMC
Habari za Siasa

Dk. Semesi ateuliwa kuwa mkurugenzi mpya NEMC

Spread the love

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Dk. Immaculate Sware Semesi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kabla ya uteuzi huu Dk. Semesi alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu na anachukua nafasi ya Dk. Samuel Gwamaka Mafwenga ambaye amemaliza muda wake.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imesema uteuzi huo umeanza tarehe 5 Januari 2024.

Dk. Semesi awali alikuwa kada wa Chadema na kuteuliwa na chama hicho kuwa Mbunge wa viti maalumu kuanzia mwaka 2015 hadi 2020.

Aidha, Juni 2020 Dk. Semesi (Kilimanjaro ), na wabunge wenzie wawili Anna Gidarya (Manyara ) na Latifa Chande (Lindi)  waltangaza kuachana na CHADEMA na kuomba kujiunga na CCM wakisema wamejionea kwa macho yao kazi iliyofanywa na serikali ya awamu ya tano wakati huo ikiwa chini ya Hayati Rais John Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!