Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lugangira: Matumizi ya mitandao katika uchaguzi yaingie kwenye sheria
Habari za Siasa

Lugangira: Matumizi ya mitandao katika uchaguzi yaingie kwenye sheria

Neema Lugangira
Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalumu, Neema Lugangira (CCM) ameshauri mswada wa sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi uwe na ibara inayozungumzia masuala ya matumizi ya mitandao katika uchaguzi ikiwemo akili mnemba (Artificial Intelligence – AI). Anaripoti Selemani Msuya …(endelea).

Lugangira ametoa ushauri huo jana Alhamisi jijini Dar es Salaam wakati  akichangia kwenye mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa unaoshirikisha wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kujadili miswada ya sheria za uchaguzi na mswada wa sheria za vyama vya siasa.

Alisema Novemba 2023, Jumuiya ya Tume za Uchaguzi Afrika ilipitisha Mwongozo wa Matumizi ya Mitandao katika Uchaguzi barani Afrika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania ni Mjumbe katika Jumuiya hiyo, hivyo itakuwa sio jambo jema kutunga sheria ambayo inakinzana na maazimio hayo.

“Mswaada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi haijagusia kabisa suala la Matumizi ya Mtandao katika Uchaguzi, jambo ambalo limeshathibitika kuwa moja ya maeneo yenye changamoto kubwa katika chaguzi zetu,” alisema.

Alisema ni lazima kuangalia pia athari za teknolojia mpya kama akili mnemba katika Uchaguzi kwa kuwa tayari dunia imekwenda huko.

“Napenda kushauri na kusisitiza Sheria hii ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi uhakikishe inaongezwa Ibara Mpya katika eneo hili la Matumizi ya Mitandao katika uchaguzi sababu Jumuiya ya Tume za Uchaguzi Afrika ambapo Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania ni Mjumbe, alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!