Sunday , 12 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tshisekedi aongoza kwa 81%, Katumbi 15% uchaguzi DRC
Habari za SiasaKimataifa

Tshisekedi aongoza kwa 81%, Katumbi 15% uchaguzi DRC

Felix Tshisekedi
Spread the love

TUME ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, CENI, imetoa matokeo zaidi ya awali ya uchaguzi wa rais, yakionesha rais Felix Tshisekedi anaongoza kwa mbali, akifuatiwa na mfanyabiashara Moise Katumbi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Matokeo yaliyotangazwa na CENI kufikia sasa yanatokana na takriban kura milioni 1.9, kati ya jumla ya wapiga kura milioni 44 waliojiandikisha katika nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati yenye ukubwa sawa na eneo la Ulaya Magharibi na yenye wakazi zaidi ya milioni 100.

Ceni alisema Tshisekedi mwenye umri wa miaka 60, aliye madarakani tangu 2019 na anayewania muhula wa pili wa miaka mitano, alikuwa anaongoza kwa zaidi ya asilimia 81 ya kura.

Alikuwa akifuatiwa kwa mbali na mfanyabiashara tajiri na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga Moise Katumbi (58), akiwa na zaidi ya asilimia 15 ya kura na mtendaji mkuu wa zamani wa mafuta Martin Fayulu (67), kwa zaidi ya asilimia moja.

Wapinzani wengine karibu 20, akiwemo Denis Mukwege, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwenye umri wa miaka (68), walishindwa kupata asilimia moja.

Ceni haijatangaza idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa tarehe 20, 21 Desemba lakini bado imekuwa ikitoa matokeo hatua kwa hatua tangu Ijumaa, ambayo ni pamoja na uchaguzi wa wabunge, mikoa na mitaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!