Saturday , 11 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Mkuu: Uchaguzi DRC umekuwa wa machafuko
Habari za SiasaKimataifa

Askofu Mkuu: Uchaguzi DRC umekuwa wa machafuko

Spread the love

Katika misa yake ya Krismasi, Askofu Mkuu wa Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Kardinali Fridolin Ambongo ameelezea jana Jumapili jioni kuwa uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita nchini humo ni kama “machafuko makubwa yaliyopangwa”.

Kanisa Katoliki lienye ushawishi mkubwa na kijadi linakosoa mamlaka nchini DRC, limetoa tamko hilo wakati tume ya uchaguzi ikiendelea kutoa matokeo ya uchaguzi wa rais. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

“Kwa shauku, kwa dhamira, wengi wetu tulijitokeza kueleza mapendeleo yetu kidemokrasia,” ametangaza Kardinali Fridolin Ambongo mbele ya waumini waliokusanyika katika kanisa kuu la Notre-Dame du Kongo, katika wilaya ya Gombe huko Kinshasa.

Felix Tshisekedi

“Lakini ole ameongeza, “kile ambacho kingekuwa sherehe kubwa ya maadili ya kidemokrasia kiligeuka kuwa mfadhaiko kwa wengi.”

“Uchaguzi ulikuwa machafuko makubwa yaliyopangwa. Nyote ni mashahidi wa hilo”, alisema askofu huyo mkuu, ambaye alitaja picha zisizoweza kuvumilika akizungumzia video inayoonyesha shambulio dhidi ya mwanamke aliyepigwa kikatili na kudhalilishwa kwa sababu alipigia kura upinzani.

“Tunatoa taswira gani ya nchi yetu duniani? Tunawezaje kuwa na tabia chafu zisizovumilika kama hizi?”, amesema kasisi huyo, katika ujumbe wake alioutoa kwanza kwa Kifaransa, kisha kwa Lingala.

Takriban wapiga kura milioni 44, kati ya takriban wakazi milioni 100 wa DRC, nchi kubwa zaidi ya Kikatoliki barani Afrika, waliitwa kumchagua rais wao, wabunge wao wa kitaifa na mikoa na madiwani wao wa manispaa siku ya Jumatano.

Mkuu wa nchi anayemaliza muda wake, Félix Tshisekedi, anawania muhula wa pili dhidi ya wagombea wengine 18, ambao baadhi yao wameshutumu “machafuko” na “makosa” ambayo wanaamini yaliharibu uchaguzi.

Baadhi wanapanga maandamano Jumatano ijayo, wengine wakitaka uchaguzi ufutiliwe mbali moja kwa moja.

Miongoni mwa wapinzani hao ni pamoja na Moïse Katumbi, gavana wa zamani wa mkoa wenye madini wa Katanga (kusini-mashariki), Martin Fayulu, ambaye anadai ushindi uliibiwa kutoka kwake katika uchaguzi wa mwaa 2018, na Denis Mukwege, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa huduma yake aliyoitoa kwa waathiriwa wanawake waliobakwa wakati vita vilikuwa vikipamba moto nchini DRC.

Matokeo ya mikoa

Kutokana na matatizo mengi ya vifaa, muda wa kupiga kura uliongezwa na tume ya uchaguzi (CENI).

Uchaguzi huo ulimalizika rasmi siku ya Alhamisi jioni lakini uliendelea hadi wikendi katika maeneo ya mbali ya mikoa kadhaa.

“Kwa sasa, ninawaomba muwe waangalifu na wenye kujizuia,” Kardinali Ambongo alisema.

Siku moja kabla ya uchaguzi, balozi 15 zilitoa wito kwamba zinasubiri ripoti kutoka kwa jumbe mbalimbali za waangalizi, hasa ile ya misheni ya pamoja ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiprotestanti, ambayo inaweza kuwasaidia kutathmini dosari zilizojitokeza na kutathmini athari zake katika uaminifu wa chaguzi hizi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!