Wednesday , 15 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wajawazito wadaiwa kujifungulia sakafuni, Serikali yatoa kauli
AfyaTangulizi

Wajawazito wadaiwa kujifungulia sakafuni, Serikali yatoa kauli

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
Spread the love

BAADHI ya akina mama wajawazito katika Kituo cha Afya cha Buzuruga, kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza, wanadaiwa kujifungulia chini kwenye sakafu kutokana na uhaba wa vitanda. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa hizo zimesambaa hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii, huku kukiwa na picha zinazoonesha baadhi ya  wajawazito wakiwa katika chumba kinachodaiwa kuwa cha kujifungulia huku wengine wakiwa wamelala chini wakisubiri huduma.

Inadaiwa kuwa, picha hiyo imepigwa na mjamzito mmoja aliyeingia na simu kwa siri baada ya uongozi wa kituo hicho kupiga marufuku ya kuingia na simu ili kuzuia watu wasipige picha.

Hata hivyo, leo tarehe 18 Disemba 2023, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Wakili Kiomoni Kibamba, amekanusha uwepo wa tukio hilo akidai hakuna mjamzito anayejifungulia chini kwa kuwa vitanda vimeongezwa kituoni hapo.

Taarifa hiyo imedai, awali kituo hicho kilikuwa na vitanda vitatu kwa ajili ya kujifungulia kitendo kilicholeta changamoto hivyo Serikali iliongeza hadi kufikia sita.

“Hivyo kwa maelezo hayo, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inapenda kuuhakikishia umma kuwa katika Kituo cha Afya cha Buzuruga, hakuna wakina mama wanaojifungulia chini kama taarifa ya mtandaoni inavyoeleza,” imesema taarifa ya Wakili Kibamba.

Kuhusu picha iliyosambaa mitandaoni, taarifa ya Wakili Kibamba imesema sio ya hivi karibuni kama inavyodaiwa, bali ilipigwa Septemba 2022.

Kabla ya taarifa hiyo kutolewa, MwanaHALISI Online ilimtafuta Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa njia ya simu ili kupata ufafanuzi wa tukio hilo, lakini simu yake haikupokelewa. Ilipomtafuta Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel simu yake haipatikani hewani.

1 Comment

  • Tuache kusema uongo mweupe. Baada ya video ndipo ukaongeza vitanda. Mbona takwimu hukutumia kutuambia walikuwa wangapi na ukakubali kulikuwa na ongezeko la wajawazito. Hivi siyo vitu vya kuficha.
    Mama hawezi kuongeza hospitali mkiendelea kudanyanya hivi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Madeleka aibwaga Jamhuri kesi za kubambikiwa

Spread the loveWakili Peter Madeleka ameshinda rufaa yake namba 263 ya mwaka...

Habari za SiasaTangulizi

Sheikh Ponda ataka kura ya maoni kuamua hatma ya muungano

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

Afya

Mbunge ataka huduma Ultrasound itolewe bure kwa wajawazito

Spread the loveMBUNGE wa Viti Maalum, Esther Malleko, ameitaka Serikali kutoa bure...

Afya

Vituo 13 vyasitishiwa mkataba madai kutaka kupiga bilioni 4 za NHIF

Spread the loveVITUO vya kutoa huduma za afya 13, vimesitishiwa mikataba ya...

error: Content is protected !!