Tuesday , 21 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020
Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020

Sheikh Ponda Issa Ponda (katikati)
Spread the love

KATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amesema changamoto zilizojitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, kama hazitajadiliwa kwa uzito na kutafutiwa mwarobaini, huenda zikatijitokeza katika chaguzi zijazo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Sheikh Ponda ametoa kauli hiyo leo tarehe 30 Novemba 2023, akizungumza na MwanaHALISI kwa njia ya simu.

Kiongozi huyo wa kidini amedai kuwa, kinachoendelea sasa ni upande wa Serikali kutoa kauli za kutaka maridhiano kufuatia changamoto hizo zilizojitokeza ikiwemo madai ya baadhi ya wananchi kujeruhiwa, kupoteza maisha na wagombea kuenguliwa, bila ya kuchukua hatua za kutengeneza mazingira mazuri ili zisijirudie.

“Ukweli ni kwamba, kama yale madhila yaliyotokea 2020 yanazungumzwa katika lugha kama vile ya kupuuza, sababu watu wanaoonesha hisisa zao kuhusu matatizo yaliyokuwepo kwenye uchaguzi, wanasema tusameheane tusitonesehe vidonda,” amesema Sheikh Ponda.

Sheikh Ponda amesema “lakini kuna watu wameuawa hapakuwa na jambo la kuchukuliwa hatua zozote zile, walioathirika hawajalipwa fidia. Serikali haijaweka mikakati ya pamoja kuhakikisha hili halitatokea tena kwenye uchaguzi, badala yake inasema tusameheane.”

Wakati Sheikh Ponda akitoa kauli hiyo, Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imechukua hatua mbalimbali kukutana na vyama vya siasa hususan vya upinzani, ili kutafuta maridhiano kwa lengo la kutafuta suluhu ya madhila yaliyojitokeza katika demokrasia hususan wakati wa uchaguzi.

Tayari Serikali imewasilisha bungeni jijini Dodoma, marekebisho ya sheria za uchaguzi, ili kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na wadau kwa ajili ya kuboresha mazingira ya chaguzi zijazo.

“Kama hayatajadiliwa kwa uzito unaotakiwa, matokeo yake tutaingia kwenye uchaguzi katika hali hiyo. Ili kusaidia tatizo kupungua inabidi yawekewe kipaumbele,” amesema Sheikh Ponda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

error: Content is protected !!