Tuesday , 21 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ulega amtumbua mkurugenzi uvuvi
Habari za SiasaTangulizi

Ulega amtumbua mkurugenzi uvuvi

Stephen Lukanga
Spread the love

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameagiza kuondolewa katika nafasi yake Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi, Stephen Lukanga baada ya kushindwa kupanga na kutekeleza mikakati thabiti ya kukomesha uvuvi haramu nchini.

Prof. Mohamed Sheikh

Ameagiza nafasi hiyo apewe aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani, Prof. Mohamed Sheikh. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akimkabidhi vifaa vya uvuvi mmoja wa Wanufaika wa mkopo wa boti katika tukio la kukabidhi boti kwa wavuvi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 28 Novemba 2023.

Waziri Ulega ametoa uamuzi huo wakati akikabidhi boti 11 zenye thamani ya Sh 1. 85 bilioni zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa mkopo kwa wavuvi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 28 Novemba 2023.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi boti kwa wavuvi wa Dar es Salaam katika tukio la kukabidhi boti kwa wavuvi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 28 Novemba 2023.

Ulega amefikia uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wadau wa uvuvi mkoani Dar es Salaam kuhusu kukithiri kwa vitendo vya uvuvi haramu  katika ukanda Pwani hususani Dar es Salaam.

Tarehe 4 Oktoba 2023 akiwa mkoani Mwanza katika Soko la Lumumba, Ulega alimpa mwezi mmoja Kaimu Mkurugenzi huyo kuhakikisha anapanga na kutekeleza mikakati thabiti ya kukomesha uvuvi haramu nchini ambao kwa muda umekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya sekta ya uvuvi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari za SiasaKimataifa

Kiongozi Mkuu Iran amteua mrithi wa Rais Ebrahim

Spread the loveKiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei,...

error: Content is protected !!