Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Biashara TPA yajivunia Zimbabwe kuwa soko jipya mizigo ya magari bandari Dar
Biashara

TPA yajivunia Zimbabwe kuwa soko jipya mizigo ya magari bandari Dar

Spread the love

KAMPENI ya kuitangaza bandari ya Dar es Salaam kimataifa imetajwa kuanza kuzaa matunda baada ya wafanyabiashara na wakazi wa Zimbabwe kuichagua bandari hiyo kupitisha mizigo mbalimbali hususani magari. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hatua hiyo imetajwa kuendelea kuvutia wateja wengi wa kimataifa kuitumia bandari ya Dar es Salaam na kuilazimu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufungua ofisi katika jiji la Harare ili kurahisisha utoaji huduma kwa wateja wake.

Hayo yamebainishwa wiki iliyopita na Afisa Uhusiano Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Levina Kato wakati akiwasilisha mada kwenye Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofanyika mkoani Lindi.

Kati alisema mbali na kampeni iliyofanywa na mamlaka hiyo, baada ya nchi jirani ikiwamo Afrika Kusini ambako Zimbabwe walikuwa wanatumia kupitisha magari yao, wamepitisha sheria ambazo zinaongeza gharama kwa waagizaji magari.

“Walipitisha sheria ya kuzuia magari hayo mapya yasipitishwe kwenye barabara zao hivyo wateja wakawa wanatumia gharama kusafirisha mzigo kupitia car carrier kwa sababu lazima anayepakia magari alipwe.

“Kwa kuwa ni gharama kubwa kwao, wakaamua kuchagua bandari za Tanzania ili wayaendeshe wenyewe magari hayo badala ya kupitia Afrika Kusini na Zambia,” alisema.

Aidha, aliongeza kuwa TPA imeendelea kuboresha bandari mbalimbali nchini ikiwamo Lindi ambako sasa mkandarasi yupo ‘site’ kuboresha bandari ya uvuvi.

Mbali na maboresho hayo kwenda sambamba na bandari ya Mtwara, Kato alisema kwa upande wa Mwanza mamlaka hiyo inaboresha bandari za mkoa huo ili ziweze kuhudumia vema sokola Uganda kupitia eneo maarufu la biashara Port Bell.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Biashara

Meridianbet watoa msaada wa chakula Chamazi

Spread the love  JUMAMOSI ya leo Meridianbet wametua pale Chamazi Magengeni kwaajili...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB ‘yafunga ndoa’ na wanawake wanaomiliki shule, vyuo Tanzania

Spread the loveBENKI ya NMB imeingia makubaliano rasmi (MoU) na Chama cha...

Biashara

Cheza kasino sloti ya Fruit O Rama malipo unayapata kwa njia 10

Spread the love Karibu kwenye burudani ya kasino ya mtandaoni isiyozuilikayenye kutawaliwa...

error: Content is protected !!