Wednesday , 15 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Sera mpya ya elimu yafuta darasa la saba, vigezo kusomea ualimu form VI
ElimuTangulizi

Sera mpya ya elimu yafuta darasa la saba, vigezo kusomea ualimu form VI

Spread the love

SERIKALI imekamilisha kazi ya mapitio ya mitaala ya elimu kuanzia ngazi ya msingi, sekondari hadi ualimu, huku ikiendelea na mapitio ya mitaala na program mbalimbali ngazi ya elimu ya kati na juu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 2 Novemba 2023, bungeni jijini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akitoa taarifa ya uidhinishwaji wa sera mpya ya elimu ya 2014, toleo la 2023.

Waziri Majaliwa ametaja maeneo yaliyofanyiwa marekebisho katika mitaala hiyo, ikiwemo elimu ya lazima kuwa ya miaka 10, elimu ya msingi kuwa miaka sita, elimu ya sekondari ya chini kutolewa kwa miaka minne na mtihani wa darasa la saba kufutwa, ambapo utekelezaji wa maboresho hayo utaanza 2027.

Amesema maboresho hayo yakianza kufanya kazi baada ya sera mpya kuzinduliwa, watakaoruhusiwa kusomea ualimu ni wale waliohitimu kidato cha sita na kuendelea, badala ya utaratibu uliopo sasa wanaochukuliwa wahitimu kuanzia kidato cha nne.

“Elimu ya amali kwa maana ya ufundi na mafunzo stadi, kuanza kutolewa kuanzia kidato cha kwanza. Elimu ya ualimu kuanza kutolewa kwa wahitimu waliomaliza kidato cha sita na kuendelea,” amesema Waziri Majaliwa.

Waziri Majaliwa amesema sababu ya marekebisho hayo ni utekelezaji wa agizo la rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kufanya mapitio ya sera na mitaala ili ijikite kutoa elimu ya ujuzi badala ya taaluma pekee.

Sababu nyingineni mfumo wa elimu kujikita zaidi kwenye elimu ya jumla na kukosa fursa za elimu na mafunzo kwa kuzingatia mahitaji na njia za ujifunzaji. Mitaala kutokidhi mahitaji ya mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisanyansi na teknolojia. Mfumo usiomadhubuti na ithibatri ya elimu na upungufu wa nguvu kazi.

“Kwa kuzingatia maelekezo ya Rais Samia, Serikali imekamilisha mapitio ya sera ya elimu na mafunzo ya 2014 na kuandaa sera mpya ya elimu na mafunzo ya 2014 toleo la 2023, sera hii mpya imezingatia maelekezo ya Rais na maoni ya wadau mbalimbali,” amesema Waziri Majaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Madeleka aibwaga Jamhuri kesi za kubambikiwa

Spread the loveWakili Peter Madeleka ameshinda rufaa yake namba 263 ya mwaka...

Habari za SiasaTangulizi

Sheikh Ponda ataka kura ya maoni kuamua hatma ya muungano

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

Elimu

Waziri SMZ akoshwa na kazi za Global Education Link

Spread the loveSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar SMZ imesema itaendesha msako na kuzifutia...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wizara kutumia Sh. 3.5 bilioni kuchunguza afya ya akili, nguvu za kiume

Spread the loveWIZARA ya Afya, imepanga kutumia Sh. 3.50 bilioni, kwa ajili...

error: Content is protected !!