Saturday , 4 May 2024
Home Kitengo Michezo Wateja wa betPawa wajishindia bilioni 53.8
Michezo

Wateja wa betPawa wajishindia bilioni 53.8

Spread the love

Wateja 333,706 wa kampuni ya Michezo ya kubashiri betPawa wameweka rekodi ya ushindi katika mchezo huo baada ya kujishindia Sh 53.8 bilioni ndani ya siku 10. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Wateja hao walisherehekea ushindi katika mchezo huo wa kubashiri kwa usahihi kwenye michezo kati ya Jumamosi tarehe 21 na Jumatatu tarehe 30 Oktoba mwaka huu.

Meneja wa betPawa nchini Borah Ndanyungu alisema mshindi wa kwanza aliyejinyakulia kitita kikubwa kuliko wote, alishindia Sh 372.9 milioni kwa dau la Sh2,200, ikiongezewa na bonasi ya ushindi ya asilimia 645 kwenye mechi 50 alizobashiri.

“Hii imedhihirisha kauli mbiu ya ‘betPawa pesa kidogo’, ushindi mkubwa (Bet Small, Win BIG) kwa jumla wateja 3,738 wa betPawa Tanzania walibadilishwa kuwa mamilionea kwa kipindi cha ndani ya siku 10.

“Kutokana na idadi hii kubwa ya washindi ambayo haijawahi kutokea ilisababisha ucheleweshaji wa malipo katika tasnia nzima ya michezo ya kubashiri. Kwetu betPawa kuwa na washindi wengi kumesababisha akaunti zetu za mitandao ya simu kulazimika kuongezwa kiwango cha pesa kila mara kulingana na kiwango cha juu kinachoruhusiwa kwa siku,” alisema na kuongeza kuwa;

“Hata hivyo tunafanya kazi saa 24 ili kumalizia malipo ya washindi wachache waliosalia.”

Aidha, Ndanyungu alisema hakuna mtu bora kuliko wateja wa betPawa ambao wamefanikiwa kupata ushindi mkubwa, na katika kipindi hiki cha siku 10 wameshinda zaidi kuliko hapo awali.

“Tunafahamu idadi kubwa ya ushindi umesababisha ucheleweshaji katika tasnia nzima ya michezo ya kubashiri na sisi betPawa tunafurahi kuwa tayari tumeweza kulipa washindi wengi tayari mpaka sasa. Tunafanya kazi bila kuchoka ili washindi wachache waliobakia mwisho walipwe,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

error: Content is protected !!