Tuesday , 14 May 2024
Home Kitengo Biashara Muunganiko Twiga, Tanga Cement wakataliwa tena mahakamani
BiasharaHabari Mchanganyiko

Muunganiko Twiga, Tanga Cement wakataliwa tena mahakamani

Spread the love

Baraza la Ushindani (FCT) la Tanzania limefutilia mbali uamuzi wa Tume ya Ushindani (FCC) uliotolewa  tarehe 28 Februari mwaka huu wa kuiruhusu Scancem International ya kutwaa asilimia 68.33 ya hisa katika Tanga Cement PLC bila masharti yoyote. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Katika uamuzi wake wa tarehe 16 Oktoba 2023,  FCT chini ya uenyekiti wa Jaji Fatma Maghimbi, iliamua kwamba madhali FCT ipo kwa ajili ya kusimamia na kurekebisha mwenendo na uamuzi wa FCC, haikuwa sahihi kuwapo maamuzi mawili yanayopingana kutoka kwenye vyombo hivyo katika suala moja, ikizingatiwa FCT ilipata awali kuzuia muungano wa kampuni hizo.

Jaji Maghimbi aliyeshirikiana na wajumbe Dk. Onesmo M. Kyauke na Dk. Godwill G. Wanga walisema haiwezekani chombo kilicho kikubwa zaidi  (FCT uamuzi wa tarehe 6 Aprili 2022) kwenye suala hilo hilo upingwe na chombo kilicho kidogo zaidi (FCC).

Walikuwa wanatoa uamuzi kwenye shauri lililofunguliwa na Peter Hellar dhidi ya FCC, Scancem International DA, Fayaz Bihojani, Wiilliam Erion a Hakan Gurdan, kutaka wajibu maombi wajieleze mbele ya baraza hilo, kwa nini wasichukuliwe hatua kwa kulidharau baraza katika maamuzi yake.

Dk. Onesmo M. Kyauke

Hata hivyo, Jaji Maghimbi na wajumbe wa FCT walisema wajibu maombi si wa kulaumiwa kwa kilichotokea, japokuwa ni kweli kwamba maamuzi mawili tofauti hayawezi kusimama kwenye soko moja.

Swali linabaki, kipi kifanyike?

Deodatus Nyoni, Wakili Mwandamizi wa Serikali akiiwakilisha FCC alipendekeza kwamba ili kupata suluhu ya hali husika, Baraza lifute uamuzi wa FCC wa Februari 28, 2023 na kutoa ruhusa kwa wajibu maombi kuwasilisha upya ombi la Baraza kupitia upya uamuzi wa Baraza hili wa tarehe 23 Septemba 2022,” wakasema kwenye uamuzi uliosomwa na Jaji Maghimbi.

Wakihitimisha, walikubaliana na wakili huyo, wakisema kwamba baraza hilo halipo kwa nia ya kuvuruga FCC wala kuchelewesha wawekezaji tarajiwa, bali kulinda na kukuza ushindani kwenye biashara na kulinda walaji, walisema muda uliotumiwa kuwasilishwa kwa ombi jipya la utwaaji hisa ulikuwa mfupi.

Hivyo hawadhani mazingira ya uchumi, biashara yalikuwa yamebadilika, wakaongeza kwamba angalau kiwe kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa msingi huo, FCT ilibatilisha ombi la kuungana kampuni husika namba CBC. 127/359/144.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Moduli ya kuwasilisha rufaa za zabuni kieletroniki kuanza Julai

Spread the loveMamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imesema moduli...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mshindi ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ akabidhiwa trekta

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imehitimisha msimu wa tatu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hati Fungani ya NMB Jamii yaanza kuuzwa Soko la Hisa London

Spread the loveBenki ya NMB imetanua wigo wa kushiriki katika masoko ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Vituo 13 vyasitishiwa mkataba madai kutaka kupiga bilioni 4 za NHIF

Spread the loveVITUO vya kutoa huduma za afya 13, vimesitishiwa mikataba ya...

error: Content is protected !!