Sunday , 12 May 2024
Home Kitengo Biashara NMB yazindua huduma maalum kwa ajili ya wastaafu
Biashara

NMB yazindua huduma maalum kwa ajili ya wastaafu

Spread the love

BENKI ya NMB imeanzisha mpango maalum wenye masuluhisho mahususi kwa ajili ya kuwahudumia wastaafu na wastaafu watarajiwa unaoitwa NMB Hekima Plan. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Utaratibu huu ambao lengo lake kubwa ni kusaidia kuenzi mchango mkubwa wa watumishi hao katika ujenzi wa taifa umezinduliwa rasmi leo Jumatatu jijini Dodoma wakati wa warsha maalum kwa ajili ya kuwaelimisha kifedha na kuwaandaa kukabiliana na changamoto za maisha baada ya ajira.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa programu hiyo mpya ambayo kauli mbiu yake ni “Staafu Kifahari” alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako.

Katika hotuba yake, kiongozi huyo alibainisha kuwa mashuruhisho hayo na programu yake ya elimu ni wazo kubwa na mtambuka katika jitihada za taifa kuboresha maisha ya wazee wote nchini. 

Aliongeza kuwa pia ni suala la thamani kwa azma ya Serikali ya kuboresha sekta ya hifadhi ya jamii na kuhakikisha kuwa wastaafu si tu wanaishi maisha bora na ya furaha lakini pia kuhakikisha wanaendelea kuchangia juhudi za ujenzi wa taifa.

“Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uendeshaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii na kuboresha mazingira ya uwekezaji nchni ili wastaafu waweze kuchangamkia fursa zinazoletwa na taasisi za fedha kama huu mpango wa NMB Hekima Plan,” Prof Ndalichako alisema.

 Akisisitiza umuhimu wa wastaafa kuwa na nidhamu ya fedha na matumizi ya pensheni zao, waziri huyo alibainisha kuwa hatua zinazochukuliwa na Serikali kuiimarisha sekta hiyo ni pamoja na kuboresha mifuko ya hifadhi ya jamii na utoaji wa huduma kwa ujumla.

 Hii ni pamoja na kupunguza kwa kiasi kikubwa cha madeni ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kupitia hatifungani maalum ambayo mwaka 1999 yalikuwa ni jumla ya Sh trilioni 4.6.

 “Serikali pia imefuta kiasi kikubwa cha madeni yake kwa PSSSF kwa kulipa TZS bilioni 500 kati ya TZS bilioni 982 ilizokuwa inadaiwa,” Prof Ndalichako aliwaambia wastaafu zaidi ya 400 wa Dodoma walioshuhudia uzinduzi wa programu hiyo.

 Aidha, alisema uwekezaji unaofanywa kubuni masuluhisho ya kidijitali na michango ya wadau kama Benki ya NMB yatasaidia si tu kuwahudumia wastaafu lakipi pia upatikanaji wa huduma kwa watu wote.

 Aliongeza kuwa yeye binafsi na Serikali kwa ujumla wanatambua changamoto za kifedha ambazo wastaafu mawekuwa wakikumbana nazo ikiwemo  kukosa uwezo wa kupangilia mapato na matumizi ya fedha zao, kupungua kwa kipato cha mwezi, kukosa usalama wa fedha pamoja na nyingine nyingi za kimaisha.

 “Niwasihi washiriki wa warsha hii na wastaafu wengine kuzingatia mafunzo na maarifa mtakayopewa na wataalum ili muweze kuzikabili changamoto hizi.”

 Katika maelezo yake kuhusu programu nzima ya masuluhisho hayo, Mkuu wa Idara ya Huduma na Biashara wa benki hiyo, Vicky Bishubo, alinena maneno yafuatayo: “Tumekuwa benki kiongozi katika kila kitu na kwenye kutoa huduma bora kwa wastaafu na tunaendelea kuboresha huduma zetu kwa ajili yao kupitia maarifa na rasilimali fedha.”

 Aidha, alisema masuluhisho yaliyomo kwenye NMB Hekima Plan ni pamoja na mikopo mbalimbali ikiwemo ile ya nyumba ambapo mkopaji anaweza kupata hadi Sh bilioni moja.

 Kupitia utaratibu huu wastaafu watapewa pia elimu ya ustawi wa afya na usalama wa fedha zao huku wakionyeshwa fursa mbalimbali za uwekezaji.

 Afisa huyo mwandamizi alisema NMB Hekima Plan ina na bima za afya na mali za gharama nafuu na bei shindani sokoni.

 Zipo pia akaunti maalumu zisizokuwa na makato ya mwezi ambazo zinampa nafasi mstaafu kupata mkono wa pole wa hadi Sh milioni mbili endapo yeye au mwenza wake atafariki na kumwezesha kupata kiasi kama hicho akipata ulemavu wa kudumu.

Bishubo aliwaambia washiriki wa warsha hiyo kuwa baada ya uzinduzi wa programu ya NMB Hekima Plus, zoezi la kutoa elimu litafanyika nchi nzima.

“Tutambue pia uwepo wa wastaafu watarajiwa ambao nao wameungana nasi siku ya leo. Tumeona ni vyema tuwaalike kwani ni kundi ambalo wataingia katika kustaafu muda si mrefu na ni vyema wakaanza kuandaliwa mapema kukabiliana na maisha ya kustaafu,” aliongeza.

Aidha, alibainisha kuwa NMB inaamini programu hizi zitaondoa ile hofu ya kustaafu kwa baadhi ya watumishi kwani watakuwa wameandaliwa kikamilifu kuishi vyema baada ya utumishi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Meridianbet yatoa msaada Kigamboni siku ya Mama Duniani

Spread the loveMABIBGWA wa michezo ya kubashiri kampuni yaMeridianbet imefika kigamboni leo siku...

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Biashara

Meridianbet kasino yaja na promo ya mil 200/=

Spread the love  Kimbunga Hidaya kilikuja na madhara makubwa sana katika maeneo...

Biashara

Moon of Thoth, historia ya Misri ya kale ilipofichwa ndani ya kasino

Spread the love  Nchi ya Misri imebeba karibia asilimia kubwa ya mambo...

error: Content is protected !!