Sunday , 12 May 2024
Home Kitengo Biashara Bashungwa atoa siku 4 Kivuko MV. Mara kikamilike
Biashara

Bashungwa atoa siku 4 Kivuko MV. Mara kikamilike

Spread the love

KAMPUNI  ya Songoro Marine imepewa siku 4 kuhakikisha inakamilisha ukarabati wa kivuko cha MV. Mara kinachofanya safari zake kati ya Iramba wilaya ya Bunda na Majita wilaya ya Musoma Vijijini na kuanza kutoa huduma ifikapo tarehe 15 Oktoba 2023. Anaripoti Danson Kaijage, Mwanza … (endelea)

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 11 Oktoba 2023 jijini Mwanza na  Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa alipotembelea karakana ya kutengeneza na kukarabati vivuko ya Songoro Marine Ltd, na kujionea vivuko tisa vya Serikali vinavyojengwa na kukarabatiwa na karakana hiyo.

Bashungwa amesema alipokuwa kwenye ziara Musoma Vijiji alipokea ombi la wananchi kutaka Kivuko hicho kirejeshwe kwani kimechukua muda mrefu tokea kipelekwe kufanyiwa ukarabati.

“Niwaletee habari njema wananchi wa Musoma Vijijni na visiwa ambavyo vilikuwa vinapata huduma ya kivuko cha Mv Mara kuwa ukarabati wa kivuko hicho umefikia asilimia 99 na kitakuwa kimekamilika kufikia tarehe 15 Oktoba 2023 ili kirejeshwe na kuanza kutoa huduma ya usafiri” amesema Bashungwa.

Pamoja na shughuli nyingine Bashungwa amemshukuru  Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Sh 321.9 milioni kukarabati kivuko hicho.

Aidha, Bashungwa amezitaka taasisi na mamlaka zote zinazohusika na ukaguzi na utoaji wa vibali baada ya ukarabati kuhakikisha wanakamilisha taratibu zote ndani ya siku nne ili kuwezesha kivuko hicho kurejeshwa mkoani Mara kuanza kutoa huduma.

Kadhalika, Bashungwa amevitaja vivuko vingine vinavyojengwa na kukarabatiwa katika karakana hiyo ni Rugezi Kisorya kimefikia asilimia 70, Ijinga- Kahangala – asilimia  67, Bwiro -Bukundo – asilimia  70, Nyakalilo -Kome – asilimia  55.5, Buyagu -Mbalika – asilimia 30, Mv. Nyerere – asilimia 79.5, Mv. Kilombero – asilimia  84 na Mv. Ruhuhu – asilimia 90.

Naye, Mkurugenzi wa Songoro Marine Ltd, Major Songoro ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwaamini na kupewa kazi za kujenga na kukarabati vivuko vya Serikali na ameahidi kufanya kazi kwa weledi na kwa mujibu wa mikataba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Meridianbet yatoa msaada Kigamboni siku ya Mama Duniani

Spread the loveMABIBGWA wa michezo ya kubashiri kampuni yaMeridianbet imefika kigamboni leo siku...

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Biashara

Meridianbet kasino yaja na promo ya mil 200/=

Spread the love  Kimbunga Hidaya kilikuja na madhara makubwa sana katika maeneo...

Biashara

Moon of Thoth, historia ya Misri ya kale ilipofichwa ndani ya kasino

Spread the love  Nchi ya Misri imebeba karibia asilimia kubwa ya mambo...

error: Content is protected !!