Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Biashara Bei ya mafuta ya petroli, dizeli kwa mwezi Oktoba yapaa tena
BiasharaTangulizi

Bei ya mafuta ya petroli, dizeli kwa mwezi Oktoba yapaa tena

Spread the love

BEI ya mafuta ya petroli kwa mwezi Oktoba 2023, imepanda kwa Sh. 68, huku dizeli ikiongezeka kwa Sh. 189. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mabadiliko hayo yametolewa jana tarehe 3 Oktoba 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),Dk. James Mwainyekule.

Taarifa ya Dk. Mwainyekule, imetaja sababu za ongezeko hilo ni kupanda kwa gharama zake katika soko la dunia, uamuzi wa wazalishaji wakubwa duniani (OPEC), kupunguza uzalishaji na vikwazo vya kiuchumi ambavyo Urusi imewekewa na mataifa ya magharibi.

Bei ya mafuta ya petroli katika Mkoa wa Dar es Salaam, imeongezeka kutoka Sh.3,213 iliyokuwepo Septemba 2023, hadi kufikia Sh. 3,281 itakayotumika Oktoba mwaka huu. Kwa upande wa Dizeli, katika mkoa huo bei imepanda kutoka Sh. 3,259 (Septemba), hadi kufikia 3,448 (Oktoba).

Kwa upande wa Tanga, bei ya Petroli imeongezeka kutoka Sh. 3,259 (Septemba) hadi kufikia 3,327 (Oktoba). Mafuta ya Dizeli yamepanda kutoka Sh. 3,305 (Septemba) hadi Sh. 3,494 (Oktoba).

Bei ya mafuta ya Petroli Mtwara imepanda kutoka Sh. 3,285 (Septemba), hadi kufikia Sh. 3,353 (Oktoba).

“Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani, isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo (Price cap) au kuwa chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price), kama zilivyokokotolewa kwa mujibu wa Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2023,zilizotangazwa kupitia 2 Gazeti la Serikali Na. 421 la tarehe 23 Juni 2023,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Simulizi za aladin na jini kutoka Meridianbet kasino ya Rise of the Genie 

Spread the love  Rise of the Genie ni mchezo wa kasino ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Hatuoni faida ya demokrasia

Spread the loveMwenyekiti wa Chadema, Fremaan Mbowe amesema Tanzania haijanufaika na miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ataka wananchi wasiruhusu bakora za Magufuli

Spread the loveMwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Profesa Ibrahimu Lipumba...

Biashara

Mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana yajivunia maendeleo

Spread the love  AFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji...

error: Content is protected !!